Sunday, November 24

DINI

UMOJA NA MSHIKAMANO NI SILAHA YA AMANI – MHE. OTHMAN
DINI

UMOJA NA MSHIKAMANO NI SILAHA YA AMANI – MHE. OTHMAN

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Alhaj Othman Masoud Othman amekumbusha haja ya mshikamano na mashirikiano katika Jamii, ili kujenga Taifa lenye Amani na Mafanikio. Alhaj Othman ametoa ukumbusho huo leo, mara tu baada ya Swala ya Ijumaa, alipojumuika na Waumini mbalimbali wa Kiislamu, katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Wete, Mkoa wa Kaskazini, Kisiwani Pemba. Amefahamisha kuwa jamii zote na Nchi kwa ujumla, zinahitaji kudumu katika umoja, mshikamano na maridhiano, kama ilivyokuwa ikisisitizwa na Wazee hapo zamani, kupitia juhudi zao za malezi mema kwa watoto, sambamba na kuepuka mifarakano isiyokuwa na tija, licha ya tofauti ndogo ndogo, ambazo haziwezi kuepukika maishani. “Kama si hivyo ilivyosisitizwa na wazazi wema hapo zamani, kupitia malezi mema ya watoto,...
SMZ itaendelea kusimamia mila, silka na tamaduni za Kizanzibari-Mh Hemed.
DINI

SMZ itaendelea kusimamia mila, silka na tamaduni za Kizanzibari-Mh Hemed.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kusimamia mila, silka na tamaduni za Kizanzibari ili Zanzibar izidi kusifika na Maadili mema. Alhajj Hemed ameyasema hayo wakati akiwasalimia waumini wa Mskiti wa Ijumaa Malindi Jongeani alipojumuika nao katika Ibada ya Sala ya Ijumaa. Amesema ni wajibu wa wananchi kusimamia Maadili mema yaliyoisifia Zanzibar na kuacha kuiga Maadilli ya Mataifa mengine ambayo yanakwenda kinyume na urithi wa Utamaduni wa Mzanzibari. Amesema Serikali itaendelea kuchukua hatua mbali mbali ili kusimamia Maadili na kusaidia kuondoa Mmong'onyoko wa Maadili na vitendo viovu vinavyoendelea katika Jamii. Mhe. Hemed amesema umefika wakati wazanzibari kuungana katika malezi ya watoto ...
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla amewataka wazazi na walezi  kuwasimamia vyema watoto wao katika kuwapatia elimu iliyo bora.
DINI

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla amewataka wazazi na walezi kuwasimamia vyema watoto wao katika kuwapatia elimu iliyo bora.

Wazazi na walezi wametakiwa kuwasimamia vyema watoto wao katika kuwapatia elimu iliyo bora itakayowasaidia katika maisha yao ya sasa na baadae. Akiwasalimia Waumini wa Masjid Kheir iliyoko Nyamanzi wakati wa Ibada ya Sala ya Ijumaa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla amesema ili watoto wafikie lengo la kutafuta elimu jitihada za wazazi zinahitajika ikiwemo kuwafuatilia na kujua mienendo ya watoto hao. Alhajj Hemed ameeleza kuwa Serikali inachukua jitihada mbali mbali katika kuimarisha sekta ya Elimu nchini hivyo, ushirikiano wa wazazi utasaidia kwa kiasi kikubwa watoto kupata elimu kwa urahisi. Ameeleza kuwa Taifa linahitaji wasomi waliobobea katika fani mbali mbali, wenye nidhamu na Maadili mema ambao watasaidia kutoa mawazo ya kuliletea Taifa maen...