Thursday, November 14

DINI

VIDEO: TATWAWWUE HAJJ & UMRA TRAVELLING AGENCY YATATHMINI SAFARI YAKE YA HIJJA 2023.
DINI

VIDEO: TATWAWWUE HAJJ & UMRA TRAVELLING AGENCY YATATHMINI SAFARI YAKE YA HIJJA 2023.

  NA KHADIJA KOMBO-PEMBA. Waumini waliorudi  kwenye ibada ya hijja  wametakiwa   kuendeleza  mema   waliyoyachuma katika  Hijja hiyo ili kuwa  mfano bora kwa wengine  kwa kuzingatia kwamba wema   ndio msingi  imara unaotakiwa kufanywa katika maisha ya kila siku . Akizungumza na Mahujjaj   waliosafiri kupitia taasisi ya Tattauwe pamoja na waumini wengine wa dini ya Kiislam katika kikao cha Tathmini juu ya safari ya Hijja mwaka huu  huko katika ukumbi wa Skuli ya Madungu Sekondari Chake Chake Sheikh Abdalla Hamad Salim kutoka Ofisi ya Mufti Pemba amesema  daima Mahujjaj wanatakiwa kuwa  kioo  ndani ya jamii kwa kuongoza kufanya mambo mema yanayompendeza Mwenyezi Mungu. Kwa Upande wake Mwenyekiti wa taasisi ya TATTAUWE  ambayo ni miongoni mwa taasisi zinazosafirisha Mah...
Alhajj Hemed Suleiman Abdulla amejumuika na waumini wa Masjid Riyaadh Amani katika Ibada ya Sala ya Ijumaa.
DINI

Alhajj Hemed Suleiman Abdulla amejumuika na waumini wa Masjid Riyaadh Amani katika Ibada ya Sala ya Ijumaa.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla amejumuika na waumini wa Masjid Riyaadh Amani katika Ibada ya Sala ya Ijumaa. Akiwasalimia waumini hao Alhajj Hemed amewataka wananchi kushirikiana na Serikali katika kupinga vitendo viovu nchini ambavyo vinamchukiza Allah (S.W) na kuondoa taswira ya Zanzibar. Amesema zipo njia nyingi zinazopelekea kuongezeka kwa vitendo hivyo ikiwemo kuwakaribisha watu tusiowajua dhamira na malengo yao, ambao pia  tunashirikiana nao katika harakati za kila siku. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema ulimwengu umetawaliwa na utandawazi hivyo, ni vyema kusimamia misingi ya Dini ya Uislamu katika maisha yetu ili kupunguza athari zitokanazo na utandawazi huo. Sambamba na hayo Mhe. Hemed ameeleza kuwa Serikali inaendelea na uj...
NCA yawahimiza vijana katika suala la utunzaji wa Amani
DINI, Kitaifa, vijana

NCA yawahimiza vijana katika suala la utunzaji wa Amani

NA ABDI SULEIMAN.   AFISA Uchechemuzi na mawasiliano kutoka shirika la NCA Nizar Selemani Utanga, alisema NCA limekua mastari wambele katika kuhakikisha vijana wanahamasika katika suala zima la utunzaji wa amani nchini.   Alisema msafara wa vijana kuhamaisha amani na utengemano wa jamii kupitia kauli mbiu yake “Amani Yetu, Kesho Yangu”, unawaleta pamoja mabalozi wa amani, vijana, vikundi vidogo za fedha, wanaume, wanawake, vijana, taasisi za , dini , viongozi wa dini, viongozi wa serikali, vyombo vya habari na asasi za kiraia kutoka Pemba. Msafara huu wa amani ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Amani na Utengamani wa Kijamii-Zanzibar na Tanzania Bara, unaotekelezwa na Norwegian Church Aid, ZANZIC/ KKKT DMP na Ofisi ya Mufti Zanzibar kwa ufadhili wa Ubal...
Al hajj Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameiasa jamii kuendelea kutekeleza maarisho ya Mwenyezi Mungu na kufuata mafundisho ya Mtume SAW .
DINI

Al hajj Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameiasa jamii kuendelea kutekeleza maarisho ya Mwenyezi Mungu na kufuata mafundisho ya Mtume SAW .

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Al hajj Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameiasa jamii kuendelea kutekeleza maarisho ya Mwenyezi Mungu na kufuata mafundisho ya Mtume SAW kwa kufanya yaliyo mema na kuacha mabaya yanayomchukiza Allah (S.W). Al hajj Dk. Mwinyi alitoa nasaha hizo kwenye Msikiti Mkuu wa Ijumaa Malindi, Wilaya ya Mjini alikojumuila na waumini wa dini ya Kiislamu kwenye ibada ya sala ya Ijumaa. Aliiasa jamii kuchunga familia zao na kuendeleza malezi ya pamoja badala ya kutelekeza familia kwa visingizio vya talaka, aliwataka familia wazichunge ndoa zao ili wajenge ustawi wa jamii iliyobora. “Ndani ya jamii zetu tuna mtihani mkubwa wa idadi kubwa ya wajane na wanapata shida kubwa ya maisha” Alieleza Al hajj Dk. Mwinyi. Alisema wanawake wanaoachika kw...