Thursday, January 9

DINI

VIDEO:Makala maalum: Ujio wa ZIDO kisiwani Pemba na ugawaji wa futari.
DINI, Makala

VIDEO:Makala maalum: Ujio wa ZIDO kisiwani Pemba na ugawaji wa futari.

  NA KHADIJA KOMBO-PEMBA. Mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa ukarimu na kutoa sana sadaka. Hii Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas  akisema: “Alikuwa MtumeMuhammad  (saw) ni mkarimu sana kushinda watu wote katika kufanya mambo ya kheri, na alikuwa mkarimu zaidi wakati wa mwezi wa Ramadhani. Kwani kuna fadhila kubwa unapotoa sadaka katika Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan. Katika kupata ujira huo  watu wengi ambao wamebarikiwa kuwa na uwezo ijapo mdogo hupendelea kufuata mwendo wa Bwana Mtume Muhammad , SAW  ili nao waweze kupata ujira huo . Jumuiya ya Kimataifa ya Maendeleo Zanzibar ZIDO ambayo ipo huko Makunduchi Zanzibar  yenye makao makuu yake nchini Canada  ni Jumuiya ambayo imekuwa ikitoa misaada mbali mbali kama vile uchimbaji wa Visima, kusaidia upatikanaji wa elimu kwa wato...
TAQWA yazipatia futari familia 502 zinazolea watoto mayatima Pemba.
DINI, ELIMU, Kitaifa

TAQWA yazipatia futari familia 502 zinazolea watoto mayatima Pemba.

NA ABDI SULEIMAN. TAASISI ya TAQWA Orphans Trust Tanzania imekabidhi msaada wa Futari kwa familia 502, zinazolea watoto mayatima zaidi ya 800   Kisiwani Pemba. Familia hizo ambazo zipo chini ya Jumuiya ya Tahfidhi Qurani na Maendeleo ya Kiislamu ya Ole, ambao ndio wasimamizi wakubwa wa familia zinazolea watoto hao. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, baadhi ya Familia ambazo zimekabidhiwa Futari hiyo, wameishukuru taasisi ya Taqwa kwa kutoa msaada huo, katika kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Bimkubwa Husein Hassan aliitaka taasisi hiyo, kutokuwa mwanzo wa kutoa msaada huo, bali iwe ni jambo la kawaida kila mwaka kuwasaidia mayatima. Alisema mayatima bado wanahitaji misaada kwa hali na mali, ili kuweza kujiona wako sawa na watoto wengine, zaidi kipindi...
SAUTI: FAMILIA YA ABDALLA HUSEIN RASHID YATOA YA MOYONI
afya, DINI, ELIMU, Kitaifa, Makala

SAUTI: FAMILIA YA ABDALLA HUSEIN RASHID YATOA YA MOYONI

Familia ya kijana Abdala Husein Rashid mwanafunzi wa darasa la kumi skuli ya kinyasini Wete Pemba mwenye ulemavu wa viungo yaomba msaada kwa wasamaria wema kupatiwa kigari kwa ajili ya kuendea skuli. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mama mzazi wa kijana huyo Time Kombo huko nyumbani kwake kwale gongo iliopo wilaya ya wete mkoa wa Kaskazini Pemba amesema kigari alicho nacho ni chaji hivyo maranyingi humzimikia njiani hakimfikishi skuli na hukwama njiani kwenye milima. Kwa upande wake mwalimu mkuu wa skuli ya kinyasini Asha Mbarouk Rashid nayeye hakuacha kuelezea changamoto za kijana huyo . Abdala Husein Rashid anasoma darasa la kumi Skuli ya sekondari kinyasini na anaishi kwale gongo ambapo ni kilomita 2.5 kutoka nyumbani kwao hadi Skuli anakosoma.  
Ifraj na Milele yasaidia Futari kwa Skuli 6 za Pemba.
DINI, Kitaifa

Ifraj na Milele yasaidia Futari kwa Skuli 6 za Pemba.

  NA SAID ABRAHMAN.   TAASISI ya Ifraj Zanzibar Foundation, kwa kushirikiana na Milele Zanzibar Foundation, imekabidhi msaada wa vyakula mbali mbali kwa ajili ya futari, kwa skuli sita Kisiwani Pemba za Sekondari Kisiwani Pemba.   Skuli zimepatiwa futari hiyo ni Skuli ya Sekondari Madungu, Fidel Castro, Pindua, Istiqama, Amini Islamic na Skuli ya Sekondari Dk.Salim Ahmed Salim.   Akizungumza katika hafla ya kukabidhi futari hiyo, kwa walimu wakuu wa skuli hizo, huko katika ofisi za Milele Zanzibar Foundation Mfikiwa Wilaya ya Chake Chake, Mkurugenzi wa taasisi Ifraji Zanzibar Foundation, Abdalla Said Abdalla alisema mwaka huu wamedhamiria kutoa futari kwa familia 4000 Kisiwani Pemba, ambazo zitaweza kuwasaidia katika mwezi wa Ramadhani.  ...
Taqwa Ophrans Trust yaandaa kongamano la kuchangisha futari kwa ajili ya mayatima
DINI

Taqwa Ophrans Trust yaandaa kongamano la kuchangisha futari kwa ajili ya mayatima

Wajumbe katika kongamano la kuchangisha futari Kwa ajili ya mayatima wanaoishi majumbani wakifuatilia kongamano la kuchangisha futari kwaajili ya mayatima hao lililoandaliwa na Taasisi ya kusaidia mayatima Tanzania Taqwa Ophrans Trust iliyofanyika katika Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar. Mwenyekiti wa Taasisi ya kusaidia mayatima waishio majumbani Tanzania Taqwa Ophrans Trust  dkt. Salha Mohammed  Kassim akizungumza machache na kumkaribisha mgeni rasmi mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar mama Zainab kuzungumza na kuchangisha futari Kwa ajili ya watoto mayatima waishio majumbani,hafla iliyofanyika Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar. Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar mama Zainab Kombo Shaibu akizungumza katika kongamano la kuchangi...