Wednesday, January 8

DINI

Ufunguzi wa Kongamano la Nane Zanzibar la Kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
DINI, ELIMU, Kitaifa

Ufunguzi wa Kongamano la Nane Zanzibar la Kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haitamvumilia yoyote atakaejihusisha na matendo ya udhalilishaji kwa lengo la kumaliza kabisa tatizo hilo. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dkt Hussein Ali Mwinyi ametoa kauli hiyo katika Hotuba iliyosomwa kwa Niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla wakati akizindua Kongamano la Nane la kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan lililofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar. Amesema Serikali imejipanga na inaendelea kuchukua hatua kali dhidi ya wanaojihusisha na matendo hayo ambayo yanaiathiri jamii hasa kwa vizazi vijavyo. Alhajj Dkt Mwinyi amesema imefika hatua kwa wananchi kuacha muhali na kutowaonea huruma wafanyaji wa vitendo hivyo ili kuisaidia Se...
Profesa Mnyaa akabidhi matofali 25,000 kwa ajili ya  msikiti na madrasa za Qurani jimboni kwake.
DINI

Profesa Mnyaa akabidhi matofali 25,000 kwa ajili ya msikiti na madrasa za Qurani jimboni kwake.

NA ABDI SULEIMAN. WALIMU wa Skuli, walimu wa madraza za Qurani na wasimamizi wa miskiti iliyomo ndani ya jimbo la Mkoani Kisiwani Pemba, wamesema kukabidhiwa kwa matufali 25,000 na mbunge wa jimbo la Mkoni Profesa Makame Mbarawa Mnyaa, yataweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika harakati zao za Ujenzi waliouwanza. Walimu hao wamesema tayari harakati zao za ujenzi zilikuwa zimeshakwama, kutokana na kukosekana kwa matufali pamoja na vifaa vyengine. Hayo waliyaeleza katika hafla ya kukabidhiwa matufali 25,000 kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Mkoani Kisiwani Pemba, kwa ajili ya kuendeleza na kumalizia ujenzi katika skuli mbali mbali, madrasa za Qurani na misikiti. Mwalimu Omar Makame kutoka Madrasa Rahman iliyoko Jondeni Mkoani, alimshukuru mbunge wa jimbo la Mkoani Profesa M...
WAZIRI HAROUN AKABIDHI MISAHAFU 200 KWA MASJID MUNAUWAR
DINI, Kitaifa

WAZIRI HAROUN AKABIDHI MISAHAFU 200 KWA MASJID MUNAUWAR

NA ABDI SULEIMAN. WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Haroun Ali Suleiman, amekabidhi Misahafu 200 kwa uongozi wa Masjidi Munauwari Mfikiwa Wilaya ya Chake Chake, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa mwaka wakati wa ufunguzi wa msikiti huo. Waziri huyo alisema amesema misahafu hiyo itaweza kuwasaidia waumini wa mskiti huo, pamoja na wanafunzi wanosoma katika madrasa iliyopo msikini hapo. Akikabidhi misahafu hiyo kwa niaba ya Waziri Haroun, msaidizi Katibu wa Mufti Pemba Sheikh Said Ahmad Mohamed, alisema utekelezaji wa msaada huo ni kuonesha mfano mzuri kwa jamii ikiwemo kutimiza ahadi hiyo. “siku ya ufunguzi wa msikiti wetu huu, Waziri Haroun aliahidi kusaidia misahafu na leo ameweza kutimiza ahadi yake kwa vitendo”alisem...
DINI

Ofisi ya mufti wakutana na walimu wa madrasa za dufu Kisiwani Pemba.

NA ABDI SULEIMAN. OFISI ya Mujfti Mkuu wa Zanzibar, imewataka walimu wa madrasa za dufu Kisiwani Pemba, kutochaganganyika kwa wanawake na wanaume katika shuli zao za upigaji wa dufu, kwani kufanya hivyo ni kukiuka misingi na maadili ya kiislamu. Kauli hiyo imetolewa na katibu Mtendaji Ofisi Mufti Zanzibar Shekh Khalid Ali Mfaume, wakati alipokua akizungumza na waalimu wa madrasa Pemba Mjini Chake Chake. Alisema upigaji wa dufu wa sasa umekua ukienda kinyume na maadili ya dini ya Kiislamu, kutokana na kuchanganyika kwa wapingaji wake jambo ambalo linaweza kusababisha matatizo hapo baadae. “Pamoja na upigaji wa Dufu kumeonekana kuna ukiukwaji mkubwa wa maadili, sisi tuliopewa nafasi hatuwezi kutizama haya ni kuona upigaji wa madufu unakiuka maadili ya dini"alisema. Alifahamish...