Tuesday, January 7

DINI

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS AWAONGOZA WAUMINI WA KIISLAMU KATIKA HAULI YA MAALIM SEIF
DINI, Kitaifa, Utamaduni

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS AWAONGOZA WAUMINI WA KIISLAMU KATIKA HAULI YA MAALIM SEIF

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, jana ameongoza Viongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, waumini wa Kiislam na wananchi mbali mbali katika Hauli ya kumkumbuka na kumuombea Dua maalum Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad. Dua hiyo maalum imefanyika huko Masjid Jibirili Mkunazini jijini Zanzibar na ilisimamiwa na Sheikh Abdurahman Alhabshy kwa khitma na nyiradi mbali mbali za kumuombea maghfira Marehemu Maalim Seif. Waliohudhuria katika dua hiyo ni pamoja na Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho Ndugu Juma Duni Haji, Kaimu Naibu Katibu Mkuu wake Zanzibar, Salim Abdalla Bimani, Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Khalid Ali Mfaume, Wanachama na Viongozi waandamizi wa ACT-...