Walimu na wanafunzi washauriwa kuvitumia vituo vya HUB kujiendeleza kielimu.
NA SAID ABRAHMAN.
WALIMU na Wanafunzi Kisiwani Pemba, wametakiwa kuvitumia vituo vya HUB ili waweze kujiendeleza kitaaluma.
Kauli hiyo imetolewa na Ofisa Miradi kutoka taasisi ya Milele Zanzibar Foundation Fatma Hamad, wakati akifungua mafunzo ya ELIMIKA yaliyoandaliwa na taasisi hiyo, kwa walimu wa Pemba huko katika kituo Cha HUB Kilichopo Skuli ya Sekondari Limbani Wete.
Alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha walimu kuweza kupata ujuzi wa kutumia mitandao, ili kuweza kuwafundisha wanafunzi kutumia njia ya mtandao katika masomo yao na kuwawezesha kufanya vizuri katika mitihani yao.
Aidha alifahamisha kuwa hivi Sasa mambo yamebadilika, hivyo aliwasisitiza walimu hao kuwashajihisha wanafunzi wao kutumia zaidi mitandao ...