Walimu wa skuli za msingi kisiwani Pemba watakiwa kuwa na utayari wa kuyatumia mafunzo ya Jifunze kwa hatua.
NA SAID ABRAHMAN.
MRATIBU wa Skuli za Sekondari Kisiwani Pemba Suleiman Hamad Suleiman, amewataka walimu wanaoshiriki mafunzo ya "Jifunze kwa hatua" kuwa na utayari ili wawe chachu kwa walimu wengine.
Alisema kuwa endapo walimu hao wataweza kuyafuatilia kwa umakini mafunzo hayo, watakuwa ni kigezo kikubwa kwa walimu wenzao ambao wako nyuma na kuwafanya nao waende na wakati.
Hayo aliyaeleza kwa niaba ya Ofisa Mdhamini wa Wizara ya elimu na mafunzo ya amali Pemba, Mohammed Nassor Salim, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya"Jifunze kwa hatua"(TaRL), yaliyoandaliwa na taasisi ya Milele Foundation huko katika kituo Cha science Pujini Wilaya ya Chake Chake Pemba.
Mratibu huyo alisema kuwa chanzo Cha baadhi ya wanafunzi kutoweza kusoma, kuandika pamo...