KOICA YAKABIDHI DAHALIA LA WANAWAKESKULI YA TUMBE
BAKAR MUSSA ,PEMBA
WAZIRI wa Kilimo , Umwagiliaji na mali asili Zanzibar , Shamata Shaame Khamis ameipongeza Serikali ya Korea Kusini kupitia Shirika lake la KOICA ( Korea International Cooperative Agency) kwa juhudi zake wazozichukuwa za kuisaidia Serikali ya Mapinduzi Zanzibar misaada mbali mbali ikiwemo Elimu.
Alisema Elimu ndio kitu muhimu katika maisha ya mwanaadamu kwani huwezi kufanya jambo lolote bila ya kuwa na elimu na ndio Mwaasisi wa Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964 na Rais wa Kwanza wa
Zanzibar hayati Abeid Aman Karume akatangaza kuwa Elimu itolewe bila ya malipo (Elimu bure).
Alieleza hayo huko katika Skuli ya Sekondari Chwaka Tumbe , kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Zanzibar , Tabia Maulid Mwita wakati wa hafla ya Uwekaji ...