Waziri SMZ wawafariji wanafunzi Skuli ya Utaani .
NA ABDI SULEIMAN.
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imewataka wazazi, wanafunzi na walimu wa skuli ya Utaani Sekondari, kuwa wastahamilivu na wavumilivu, na kufahamu kuwa mtihani uliotokea ni mipango ya Mwenyezi Mungu imeshaandikwa.
Imesema kutokea kwa mtihani wa kuungua kwa modo weni la wanafunzi wanawake, haitokua sababu ya kurudi nyuma kimasomo badala yake masomo yataendelea siku zote hususana kwa wanafunzi ambao wanajindaa na mitihani yao ya kidatoi cha sita.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Lela Mohamed Mussa, alipokua akizungumza na wazazi, walimu na wanafunzi huko skuli ya Utaani, kwa lengo la kuwafariji waathirika wa tukio hilo.
Alisema suala la elimu ni jambo muhimu sana kwa watoto, aliwataka wanafunzi kuzidisha juhudi katika m...