VYOMBO VYA HABARI VISAIDIE DUNIA KUPUNGUZA HOFU ZITOKANAZO NA HABARI POTOFU KWENYE MAPIGANO YA URUSI NA UKRAINE
Na Gaspary Charles.
Naiona hatari kubwa sana mbeleni ya athari za kisaikolojia ulimwenguni (world psychological effects by fake news) kutokana na kushamiri na kusambaa kwa kasi sana taarifa potofu juu ya mapigano yanayoendelea kati ya Urusi na Ukraine.
Licha ya mzozo huu kufikia hatua mbaya sana, lakini ni wazi kwamba taarifa zisizo sahihi juu ya kinachoendekea Ukraine mpaka wakati huu ndizo zimechukua nafasi kubwa masikioni mwa watu hasa kupitia mitandao ya kijamii jambo linalozidisha wasiwasi zaidi na taharuki kuwa kubwa zaidi duniani kuliko uhalisia wa jambo lenyewe lilivyo.
Kwa siku mbili mtawalia nimefuatilia kwa ukaribu vyanzo mbalimbali vya habari kutoka 'viwanja vya mapigano' na ni ukweli usiopingika kwamba hali kwasasa ni mbaya kwa maeneo hayo lakini zip...