Milele itaendelea kuekeza kwa vijana katika suala la elimu .
NA ABDI SULEIMAN
TAASISI ya Milele Zanzibar Foundation imesema kuwa itaendelea kuekeza kwa vijana katika suala la elimu kwa kuwajenga kuwa wabunifu ili waweze kuingia katika ulimwengu wa kazi.
Milele imesema kuwa ikiwa vijana watajenga ipasavyo kuwa wabunifu katika fani mbali mbali, basi wataweza kushindana na kuibuka washindi kupitia fani zao walizojengwa.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Miradi kutoka Taasisi ya Milele Zanzibar Foundation Khadija Ahemed Shariff, katika hafla ya kuwazawadia wanafunzi 64 waliofauli sita waliofaulu mchipuo na Viwapa, kutoka skuli zilizofanya vizuri zilizomo katika shehia zilizomo katika miradi ya milele.
Aidha alizitaja skuli hizo kuwa michezani msingi, sizini msingi, Pujini Msingi na Skuli ya Mnarani Makangale ambayo imeweza kupasisha wa...