(PICHA NA ABDI SULEIMAN,PEMBA)
NA ABDI SULEIMAN.
KAMBI iliyoanzishwa na Mbunge wa Jimbo la Kiwani, kwa wanafunzi wa Skuli za Msingi zilizomo ndani ya jimbo hilo, imeweza kuzaa matunda kwa kutoa Mchipuo na Vipawa Maalumu wanafunzi 20 kati ya 53 walioshiriki kambi hiyo.
Skuli zilizoshiriki katika kambi hiyo ni Kiwani Msingi, Mtangani Msingi, Tasini Msingi, Mwambe Msingi, Minazini Msingi, Mwambe Shamini Msingi.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa wanafunzi hao 20, Mbunge wa Jimbo hilo Rashid Abdalla Rashid, alisema lengo la kuanzisha kambi hiyo ni kuini viwango vya wanafunzi na kurudisha heshima ya elimu kwenye skuli zilizomo ndani ya jimbo hilo.
Alisema kufaulu kwa wanafunzi 20 ndio waondoshaji wa changamoto za elimu, kwani watahakikisha wana...