UPO umuhimu mkubwa wa kumiliki na kusajili kwa jamii kisheria
NA ABDI SULEIMAN.
AFISA Usajili ardhi na utoaji wa hati miliki kutoka Kamisheni ya Ardhi Pemba Yussuf Hamad Kombo, amesema ili kuweza kupunguza migogoro ya ardhi katika jamii na wanawake kupata haki zao kisheria.
Alisema ardhi ni rasilimali pekee ambayo inamsaidia mtu baada ya kuisajili kisheria, kwani anamuondoshea matatizo mbali mbali ikiwemo kuepusha na migogoro.
Afisa huyo aliyaeleza hayo mjini chake chake, katika mkutano wasiku moja ulioyashirikisha mabaraza ya ardhi ya wanawake Mkoa wa kusini Pemba, kupitia mradi wa uhamasiahaji wa upatikanaji wa haki za usimamizi wa ardhi kwa wanawake, unaotekelezwa na jumuiya ya PECEO kwa ufadhili wa FCS.
Alisema kamisheni ya ardhi inaongozwa na sheria saba (7)zote zinahakikisha ardhi ardhi inakuwa salama na serikali ndio mmiliki wa ar...