Bodaboda na bajaji watakiwa kuruata sheria za usalama wa barabarani
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Bi Rahma Kassim Ali amesema sekta ya usafiri wa Bodaboda na Bajaji ni sekta mpya kwa Zanzibar hivyo kuna haja ya kutoa elimu ya matumizi bora ya barabara hususani kwa waendesha bodaboda, bajaji na watumiaji wa huduma hiyo.
Aliyasema hayo wakati akifungua mafunzo kwa waendesha bodaboda katika viwanja vya Mao Zedong Mjini Zanzibar ambayo yameandaliwa na Shirika la Bima Tanzania.
Alisema usafiri huo umerasimishwa rasmin Zanzibar kwa mujibu wa sheria hivyo matumaini yake kuwa washiriki wa mafunzo hayo watapata fursa ya kueleweshwa undani wa sheria na kauni zake pamoja na kujikinga na majanga yatokanayo na ajali za barabarani.
Waziri huyo aliipongeza Jumuiya ya Bodaboda kwa kujipanga na kusimamia uundwaji wa Jumuiya yao ambayo ni kiungani...