WATOTO NI WAO LAKINI KWENDA SHULE NI LAZIMA – WAZIRI MKUU
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesemajukumu la kulea watoto na kutafuta mahitaji ni la wazazi lakini wajibu wa kuwasomesha watoto hao ni wa Serikali.
“Tulishasema, mtoto wa Kitanzania kwenda shule ni lazima. Watoto ni wao, lakini kwenda shule ni lazima. Ndiyo maana Serikali ilifuta ada katika shule zote.”
Alitoa kauli hiyo jana mchana (Jumanne, Desemba 28, 2021) wakati akizungumza na viongozi wa mkoa wa Lindi waliofika kumpokea kwenye uwanja wa ndege wa Nachingwea, mkoani humo.
Waziri Mkuu alisema ujenzi wa madarasa unaoendelea kote nchini hivi sasa, unalenga kuhakikisha kila mtoto wa Kitanzania anakwenda shule iwe ni ya msingi au ni ya sekondari. “Tunataka tuondoe kabisa tabia ya kukuta watoto wetu wakifanya biashara kwenye stendi za mabasi au nyumba za star...