Vyoo 12 vyajengwa skuli ya Ole, sasa wanafunzi waondokana na kujisaidia vichakani
NA ABDI SULEIMAN.
LICHA kupata msaada wa kujengewa Matundu 12 ya Vyoo na Mdau wa Maendeleo, lakini bado matundu hayo hayajakidhi mahitaji ya wanafunzi wa skuli ya Ole Msingi Wilaya ya Chake Chake katika suala la vyoo.
Skuli hiyo yenye wanafunzi 1849, inahitaji angalau matundu ya vyoo 50, ambalo tundu moja litaweza kutumiwa na wanafunzi 37 kwa wakati mmoja.
Matundu hayo yameweza kujengwa na mdau huyo, kufuatia taarifa iliyoatolewa na Gazeti la Zanzibar leo Toleo NO:6335 la Septemba 8/2021 ukurasa wa tano inayosema skuli ya kosa vyoo wanafunzi wajisaidia vichakani, msiktini na toleo NO:6425 Novemba 16/2021 ukurasa wa 12 na 13 inayosema Uhaba wa vyoo waikabili skuli ya ole Msingi.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, kufuatia ujenzi huo wa matundu 12 ya vyoo Mwalimu Mku...