WATOTO kusoma ni haki yao na sio kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji “Siti Habib kutoka ZLSC
NA ABDI SULEIMAN, PEMBA
WAZAZI na walimu wameshauriwa kuwalinda watoto dhidi ya udhalilishaji na kuepuka kuwa miongoni mwa watendaji wa matendo hayo.
Akizungumza na wanafunzi katika skuli ya Maandalizi Madungu Chake Chake, mwanasheria kutoka Kituo cha Huduma za Sheria (ZLSC) Pemba Siti Habib Mohamed alisema, ipo haja ya kuwasaidia watoto wasifanyiwe udhalilishaji wanapokuwa skuli, madrasa na nyumbani.
Alisema kuwa, ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha watoto wanakuwa salama muda wote, huku wazazi na walimu wakiepuka kuwafanyia watoto hao udhalilishaji, kwani inaaminika kwamba wanakuwa kwenye mikono salama.
“Utasikia mwalimu au mzazi anambaka mtoto, kwa kweli inahuzunisha sana, kwa sababu hatujui sasa watoto waelekee wapi, zile sehemu ambazo tunaona ni salama kw...