Rais Dkt Mwinyi aweka Jiwe la Msingi skuli ya sekondari Maziwang’ombe Wilaya ya Micheweni.
NA ABDI SULEIMAN, PEMBA
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi, amsema Serikali imeanza utekelezaji wa mageuzi katika mfumo wa elimu, ili kuhakikisha vijana wanapata elimu inayowezesha kukabiliana na changamoto za mazingira yao halisi.
Rais Mwinyi aliyaeleza hayo katika viwanja vya skuli ya sekondari Maziwang’ombe Wilaya ya Micheweni, mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi skuli hiyo ikiwa ni shamra shamra za miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Alisema kuanzia mwaka 2024, Serikali itaanza majaribio ya mtaala mpya wa elimu ya sekondari, mtaala ambao utalenga kujenga ujuzi wa vijana katika fani mbalimbali kwa kuzingatia mazingira yao.
“Kwa Maziwang'ombe, hii inamaanisha vijana watapata ujuzi unaoendana na mazingira yaliotuzunguka, ikiwa...