MUFTI mkuu afungua msikiti na kuwataka waislamu kuendeleza amani
NA ABDI SULEIMAN,
MUFTI Mkuu wa Zanzibar Shekh Saleh Omar Kaabi, amewataka wananchi wa sompiya kuwa na moyo wa kushirikiana, katika kutatua matatizo ya jamii zao na maeneo ya jirani, ili amani na utulivuo iendelea kudumua.
Mfufti Mkuu aliyaeleza hayo wakati alipokua akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu na wananchi wa shehi ya Sompiya, mara baada ya kufungua mskiti kijijini hapo.
Shekh Kaabi alisema pahala patakatifu katika ardhi ni mskitini, kwani mskiti usipotumiwa kwa kusali utawasuta, hivyo unapaswa kutumiwa kufanya ibada na kuwahimiza watoto kusali.
“Tunapaswa kuutumia msiki kwa mambo mema, ikiwemo kuweka darsa mbali mbali, kuwasomesha watoto wetu mambo mema, tutumie pia kusuluhishana migogoro inayotoka katika jamii”alisema.
Naye katibu wa Muft Shekh Kh...