VIDEO: DC Mkoani alishukuruku shirika la UNESCO kwa kuiunga mkono Wilaya hio.
NA KHADIJA KOMBO-PEMBA
Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja amelishukuru shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa juhudi zake za kuiunga mkono Wilaya hio kwa miradi mbali mbali ya maendeleo ndani ya jamii.
Mkuu huyo wa Wilaya ametoa pongezi hizo huko ofisini kwake wakati alipokutana na Mkurugenzi Mkaazi na Mwakilishi wa UNESCO nchini Tanzania aliyefika Ofisini kwake huko Mkoani mara baada ya uzinduzi wa kituo cha Makuzi na malezi ya watoto huko Skuli ya Msingi Mkanyageni katika Wilaya ya Mkoani.
Amesema Serikali ya Wilaya inathamini juhudi za Shirika hilo na kuahidi kufanya kazi nao kwa pamoja ili kuinua ustawi wa jamii hasa watoto katika upatikanaji wa elimu.
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkaazi na mwakilishi wa UNESCO nchini Tanzania Bwana Tirso...