ZAIDI YA DOLA ZA KIMAREKANI BILIONI 10 KUWEKEZWA KATIKA BIASHARA YA KABONI NCHINI TANZANIA
Tanzania imepokea Makampuni zaidi ya 20 kutoka kwenye Mataifa mbalimbali Duniani ambayo yameingia mkataba wa kufanya uwekezaji katika Biashara ya hewa ya Kaboni unaotarajiwa kuwa wa thamani ya zaidi ya Dola za Kimarekani (USD) bilioni 10.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) ameyasema hayo leo alipokuwa akifunga Mdahalo wa Masuala ya Biashara ya Hewa ya Kaboni katika ukumbi wa Johari Rotana jijini Dar es Salaam.
“Mpaka sasa Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Taasisi zake za Wakala ya Huduma za Misitu Tanzania (TFS),Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) zimepokea makapuni zaidi ya 20 kutok...