MIAKA 40 JELA UJANGILI MENO YA TEMBO – LUSHOTO
Na. Jacob Kasiri - Lushoto
Mahakama Wilayani Lushoto mkoani Tanga mwishoni mwa wiki hii imewatia hatiani watuhumiwa 3 ambao ni Bw. Hassan Kashamba, Elihudi Andrew na Godson Kitau kwa makosa mawili ya kukutwa na kijihusisha (Possession and Dealing) na nyara za serikali ambazo ni meno matano ya Tembo kinyume na sheria.
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkuu wa mahakama hiyo Mhe. Rose Andrew Ngoka amewahukumu kwenda jela miaka 40 kila mmoja kwa makosa yote mawili huku kila kosa likichukua miaka 20.
Watuhumiwa hao licha ya kukutwa na meno matano ya tembo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 104, pia walikamatwa na pikipiki 2 aina ya Kinglion zenye usajili namba MC 152 CCQ na MC BWQ zilizokuwa zikitumika katika kutenda uhalifu huo.
Waendesha mashtaka kwa upande wa serikali ambao ni ...