Saturday, December 28

Kimataifa

Nchi za Afrika Mashariki zimekumbwa na tatizo kubwa la mtandao
Kimataifa

Nchi za Afrika Mashariki zimekumbwa na tatizo kubwa la mtandao

Muunganisho wa intaneti ulitatizwa ndani na karibu na mataifa kadhaa ya Afrika Mashariki siku ya Jumapili, shirika la uchunguzi wa mtandao la Netblocks lilisema, na kuongeza kuwa tukio hilo lilihusishwa na kushindwa kuathiri mifumo ya kebo ya SEACOM na EASSy chini ya bahari. Tanzania na kisiwa cha Ufaransa cha Mayotte vilikuwa na athari kubwa kwenye muunganisho wa intaneti, wakati Msumbiji na Malawi zikiona athari ya wastani, Netblocks’ ilisema kwenye jukwaa la mtandao wa kijamii la X (Zamani ikiitwa twitter). Kampuni ya mtandao ya Cloudflare ilisema kwenye moja ya akaunti zake za X inayofuatilia mwenendo kuwa kukatika kwa intaneti kunaendelea nchini Tanzania, Malawi, Msumbiji na Madagascar kutokana na hitilafu zilizoripotiwa kwenye Mfumo wa Kebo za Nyambizi wa Afrika Mashariki ...
Wanne wakamatwa kuhusiana na kutundikwa kwa sanamu ya Vinicius Jr katika daraja Uhispania
Kimataifa, Michezo

Wanne wakamatwa kuhusiana na kutundikwa kwa sanamu ya Vinicius Jr katika daraja Uhispania

  Polisi nchini Uhispania wamewakamata watu wanne wanaoshukiwa kuning'iniza sanamu ya mchezaji wa Real Madrid, Vinicius Jr, kutoka kwenye daraja la Madrid. Sanamu hiyo hiyo ilionekana Januari kabla ya mechi kati ya Real na wapinzani wao katika mji mkuu, Atletico. Ilitundikwa kwa shingo yake chini ya bendera isemayo: "Madrid inachukia Real". Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil, ambaye ni mweusi, alikumbana na dhuluma za rangi na mashabiki wa timu pinzani wakati wa mchezo wa La Liga wikendi. Klabu yake iliwasilisha malalamiko ya uhalifu wa chuki. Mechi ya Real huko Valencia Jumapili ilisitishwa katika kipindi cha pili huku Vinicius aliyekasirishwa akiwaripoti mashabiki wa upinzani kwa mwamuzi. Kufuatia mechi hiyo, ambapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 baadaye alitolewa...
VAR aliyependekeza VIN kupewa kadi nyekundu afutwa kazi
Kimataifa, Michezo

VAR aliyependekeza VIN kupewa kadi nyekundu afutwa kazi

Shirikisho la Soka la Uhispania (RFEF) limewafuta kazi Waamuzi 6 wa VAR akiwemo Mwamuzi Ignacio Iglesias Villanueva ambaye alipendekeza Vinicius Junior kutolewa kwa kadi nyekundu katika mechi ya Valencia dhidi ya Real Madrid Kwa mujibu wa vyombo vya Habari Nchini Uhispania, Shirikisho hilo halikufurahishwa na utendaji kazi wa Villanueva ambaye inadaiwa aliondoa picha iliyokuwa ikionesha mchezaji wa Valencia Hugo Duro akimkaba koo Vini Jr kwa nyuma. Villanueva alimwita mwamuzi wa kati, Ricardo de Burgos Bengoetxea kujiridhisha kwenye skrini ya VAR lakini VAR ilionyesha kipande kilichoonesha Vini Jr akimpiga Hugo usoni pekee huku kipande ambacho Duro akimkaba Vini Jr kwa nyuma kikiwa hakipo. Baada ya kujiridhisha Mwamuzi wa kati alitoa kadi nyekundu. Licha ya kuandamwa na kauli ...
TAMWA-ZANZIBAR kuadhimisha siku ya siku ya wanawake dunia tarehe 15/3/2023 kwa kuandaa kongamano litakalojadili matumizi sahihi ya teknolojia, changamoto na faida zake kwa wanawake.
Kimataifa, Wanawake & Watoto

TAMWA-ZANZIBAR kuadhimisha siku ya siku ya wanawake dunia tarehe 15/3/2023 kwa kuandaa kongamano litakalojadili matumizi sahihi ya teknolojia, changamoto na faida zake kwa wanawake.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI   Matumizi sahihi ya kiteknolojia yalete uwiano wa kijinsia Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ) kitaadhimisha siku ya wanawake dunia tarehe 15/3/2023 kwa kuandaa kongamano litakalojadili masuala ya matumizi sahihi ya teknolojia, changamoto na faida zake kwa wanawake na jamii kwa ujumla, sambamba na kuangalia umuhimu wa matumizi ya kiteknolojia katika taasisi za sheria ili kuharakisha upatikanaji wa haki. Hafla hiyo itafanyika katika ukumbi wa Umoja wa Watu wenye Ulemavu Zanzibar (UWZ) uliopo Kikwajuni kuanzia saa 2:30 asubuhi ambapo itahusisha washiriki muhimu kutoka katika taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali ambazo zinajihusisha na masuala ya kisheria, haki za binadamu, elimu na wanamtandao wa kupinga vitendo ...
MELI YA KIMATAIFA KUTOKA AUSTRALIA YATIA NANGA HIFADHI YA URITHI WA UTAMADUNI WA DUNIA MAGOFU YA KILWA KISIWANI NA SONGO MNARA.
Kimataifa

MELI YA KIMATAIFA KUTOKA AUSTRALIA YATIA NANGA HIFADHI YA URITHI WA UTAMADUNI WA DUNIA MAGOFU YA KILWA KISIWANI NA SONGO MNARA.

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyampori Tanzania (TAWA), leo  Machi 7, 2023 imepokea meli ya kimataifa ya utalii iitwayo Coral Geographer kutoka nchini Australia.   Meli hiyo yenye hadhi ya nyota tano imebeba watalii 120, ambao wametembelea Hifadhi ya Urithi wa Utamaduni wa Dunia Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara na kufanya utalii wa malikale pamoja na utalii wa fukwe.