Friday, January 31

Kimataifa

Kombe la Dunia 2022:Kikosi cha Argentina chalazimika kutumia helikopta baada ya mashabiki milioni nne kufurika barabarani kwa sherehe
Kimataifa, Michezo

Kombe la Dunia 2022:Kikosi cha Argentina chalazimika kutumia helikopta baada ya mashabiki milioni nne kufurika barabarani kwa sherehe

ashindi wa Kombe la Dunia wa Argentina walilazimika kuachana na gwaride la mabasi ya wazi huko Buenos Aires na badala yake wakapanda helikopta juu ya mamilioni ya mashabiki waliokuwa na furaha barabarani. Kikosi hicho kilionyesha kombe hilo mwanzoni mwa safari iliyopangwa ya saa nane. Lakini sherehe kwenye barabara zilizojaa zilizidi kuwa hatari, na kulazimisha kubadilishwa kwa mpango wa kutumia mabasi. "Haikuwezekana kuendelea uwanjani kutokana na idadi kubwa ya mashabiki wenye furaha," aliandika msemaji wa rais Gabriela Cerruti kupitia Twitter. Getty ImagesCopyright: Getty Images Video za mitandao ya kijamii zilionekana kuonyesha mashabiki wakiruka juu ya basi lililokuwa limebeba wachezaji wakati mmoja lilipopita chini ya daraja, huku shabiki mmoja akianguka. Serikali...
ARGENTINA YANYAKUA KOMBE LA DUNIA 2022
Kimataifa, Michezo

ARGENTINA YANYAKUA KOMBE LA DUNIA 2022

  NA EMMANUEL MBATILO TIMU ya Taifa ya Argentina imeibuka mabingwa kombe la Dunia kwa mikwaju ya Penati dhidi ya timu ya Taifa ya Ufaransa mara baada ya kutoka sare ya 2-2  kwa dakika 90 na 3-3 dakika 30 za nyongeza (extra time). Argentina ilianza kutangulia kwa mabao 2-0, mabao yaliyofungwa kipindi cha kwanza kupita kwa nyota wao Lionel Messi pamoja na Angle Di Maria na kuwapeleka mapumziko wakiwa mbele. Kipindi cha pili Ufaransa ilifanya mabadiliko ya baadhi ya wachezaji wake, mabadiliko  ambayo yalizaa matunda kwani walipata mabao mawili ya haraka kupitia kwa kijana wao nyota Kylian Mbappe na kumfanya amzidi mpinzani wake Lionel Messi kufikia mabao saba wakati mweznake akiwa na mabao sita tu kwenye michuano hiyo..
Benjamin Netanyahu: Kiongozi wa zamani wa Israel aliyerejea mamlakani
Kimataifa

Benjamin Netanyahu: Kiongozi wa zamani wa Israel aliyerejea mamlakani

Wakati Benjamin Netanyahu alipoondolewa madarakani mnamo Juni 2021 baada ya miaka 12 mfululizo akiwa waziri mkuu, waangalizi wa mambo waliitaja mwisho wa enzi, wakati wakosoaji wake walizungumza juu ya mapambazuko mapya. Bwana Netanyahu mwenyewe ingawa aliahidi kwa ukaidi: "Tutarudi!" Kama ilivyobainika kuondoka kwake kulikuwa kumebadilika sana, huku Bw Netanyahu akiinua hali mpya ya kisiasa kwa ushindi wa kuridhisha katika uchaguzi zaidi ya mwaka mmoja baadaye, kulingana na matokeo ya awali. Kwa kejeli, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 73 wa chama cha mrengo wa kulia cha Likud anaonekana kumwangusha mpinzani wake wa mrengo wa kati Yair Lapid, ambaye ndiye aliyeanzisha anguko lake. Kurejea kwake kutatia muhuri imani miongoni mwa wafuasi wake kwamba "King Bibi" ha...
Hakutakuwa na barafu Mlima Kilimanjaro ifikapo 2050
Kimataifa

Hakutakuwa na barafu Mlima Kilimanjaro ifikapo 2050

Mabadiliko ya hali ya hewa: Hakutakuwa na barafu Mlima Kilimanjaro ifikapo 2050 Saa 2 zilizopita Barafu kote ulimwenguni - ikiwa ni pamoja na zile za mwisho barani Afrika - bila kuepukika zitapotea kabisa ifikapo mwaka 2050 kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, UN inasema katika ripoti. Theluthi moja ya barafu katika maeneo ya Urithi wa Dunia wa Umoja wa Mataifa itayeyuka ndani ya miongo mitatu, ripoti ya UNESCO iligundua. Barafu za mwisho za Mlima Kilimanjaro zitatoweka kama vile barafu katika Milima ya Alps na Hifadhi ya Kitaifa ya Yosemite nchini Marekani. Zitayeyuka bila kujali hatua za ulimwengu za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, waandishi wanasema. Ripoti hiyo, ambayo hufanya makadirio kwa kuzingatia data za satelaiti, inakuj...
RAIS SAMIA SULUHU HASSANAKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA WA CHINA LI KEQIANG,BEIJING NCHINI CHINA
Kimataifa

RAIS SAMIA SULUHU HASSANAKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA WA CHINA LI KEQIANG,BEIJING NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na ujumbe aliombatana nao kwenye mazungumzo na Waziri Mkuu (Premier) wa Jamhuri ya Watu wa China Li Kegiang mara baada ya kuwasili The People Great Hall, Beijing nchini China tarehe 03 Novemba, 2022.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu (Premier) wa Jamhuri ya Watu wa China Li Keqiang mara baada ya kuwasili The People Great Hall, Beijing chini China tarehe 03 Novemba, 2022.