Euro 2020: Wachezaji hawa wana asili ya ukanda wa Afrika Mashariki
Mashindano ya Euro 2020 yanaendelea katika mjiji 11 barani Ulaya, ni mashindano yanayoshirikisha wachezaji 622 kutoka mataifa 24 barani humo. Kizuri kati ya wachezaji hawa, wako wachezaji 55 wenye asili ya Afrika wanaowakilisha mataifa ya Ulaya.
Timu ya taifa ya Ufaransa ina wachezaji 12 wenye asili ya Afrika akiwemo Ngolo Kante mwenye asili ya Mali, Kylian Mbappe (Cameroon) Karim Benzema (Algeria) na Paul Pogba (Guinea), Huku Finland na Ujerumani zikiwa na wachezaji wengi pia weye asili ya Afrika. Mfano Ujerumani ina Antonio Rudiger (Sierra Leone), Serge Gnabry (Ivory Coast), Jamal Musiala (Nigeria) na Leroy Sane, ambaye baba yake aliwahi kucheza ligi ya Ujerumani ana asili ya Senegal.
Ukiacha hao na wengine maarufu kama David Alaba nahodha wa Austria mwenye asili ya Nig...