Saturday, March 15

Kimataifa

NCHI ZILIZOENDELEA ZAOMBWA KUZISAIDIA NCHI ZINAZOENDELEA KUHIMILI MABADILIKO YA TABIANCHI
Kimataifa, Kitaifa

NCHI ZILIZOENDELEA ZAOMBWA KUZISAIDIA NCHI ZINAZOENDELEA KUHIMILI MABADILIKO YA TABIANCHI

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Hamad Hassan Chande akizungumza wakati akizindua Maonesho ya Mabadiliko ya Tabianchi Mei 18, 2021 katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Saalam yaliyoandaliwa na EU kwa kushirikiana na Tanzania. Kushoto ni Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Mhe. Manifredo Fanti. Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Mhe. Manifredo Fanti akizungumza wakati wa Maonesho ya Mabadiliko ya Tabianchi Mei 18, 2021 katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Saalam yaliyoandaliwa na EU kwa kushirikiana na Tanzania. Katikati ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Hamad Hassan Chande. Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Mhe. Manifredo Fanti akimpitisha Naibu Waziri Ofisi ya Makamu w...
UN: Vifo 745,000 vimetokona na kufanya kazi sana
afya, Kimataifa

UN: Vifo 745,000 vimetokona na kufanya kazi sana

Utafiti wa Shirika la Afya duniani (WHO) na la Kazi duniani (ILO) unaonesha kufanya kazi kwa muda mwingi katika kipindi cha mwaka 2016, kumechangia vifo 745,000. Katika utafiti wao huo, mashirika WHO na ILO kwa pamoja yanakadiria watu 398,000 wamekufa kutokana na ugonjwa wa kiharusi na 347,000 magonjwa ya moyo kwa 2016. Sababu ambayo inaoneshwa ni kufanya kazi kwa muda mrefu kunakofikia masaa 55 kwa wiki. Kati ya mwaka 2000 na 2016, idadi ya vifo vilivyotokana na magonjwa ya moyo kwa sababu ya kufanya kazi kwa muda mrefu viliongezeka kwa asilimia 42, na kiharusu asilimia 19, na mzigo mkubwa wa vifo hivyo kwa asilimia 72 unabebwa na wanaume. Maeneo ambayo yanatajwa kuwa na athari zaidi  kwa wafanyakazi wa umri wa kati au wazee ni Magharibi mwa Asia Pasifiki na Ukanda wa Kusi...
WAZIRI MKUU AKAGUA MAGOMENI QUARTERS
Kimataifa, Kitaifa

WAZIRI MKUU AKAGUA MAGOMENI QUARTERS

    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akikagua mradi wa nyumba za makazi ya waliyokuwa wakazi wa eneo la Magomeni Quarters Aprili 20, 2021, jijini Dar es salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akifafanuliwa jambo na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo nchini (TBA,) Mbunifu Majengo. Daud Kondoro, wakati alipokagua nyumba za Magomeni Quarters. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiangalia moja ya chumba, wakati alipokagua mradi wa nyumba za makazi ya waliyokuwa wakazi wa eneo hilo, Magomeni Quarters       Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akikagua mradi wa nyumba za makazi ya waliyokuwa wakazi wa eneo la Magomeni Quarters Aprili 20, 2021, jijini Dar es salaam.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mizozo inayozihusisha China,Urusi ,Iran na Korea kaskazini inatishia amani duniani
Kimataifa

Mizozo inayozihusisha China,Urusi ,Iran na Korea kaskazini inatishia amani duniani

Uliwemgu umekuwa na muda mrefu wa utulivu isipokuwa mizozo ya vita katika mataifa machache vilivyohusisha nchi katika mabara tofauti miaka ya hapo nyuma. Tangu kukamilika kwa vita vya pili vya dunia mwaka wa 1945 hapajawahi kuwa na vita vikubwa vilivyohusisha nchi nyingi kote duniani kuweza kutajwa kama vita vya tatu. Mzozo wa Kosovo miaka ya 90 na mashambulizi ya baadaye ya Marekani dhidi ya mataifa mbali mbali huko mashariki ya kati iliweza kufika tamati baada ya nchi husika kujipatia uhuru ama Viongozi waliokuwa wakipigwa vita kuondolewa madarakani hususan katika mizozo ya mashariki ya kati. Merkel suluhisho ni 'majadiliano ya wazi' Hata hivyo kuna uhasama ama migogoro baina ya nchi mbali mbali ambayo wakati mwingine huonekana kutokota na kufika...
Virusi vya Corona: Familia yangu ilitaka kunioza nikiwa na miaka 14
Kimataifa

Virusi vya Corona: Familia yangu ilitaka kunioza nikiwa na miaka 14

Ripoti mpya ya Unicef iliyotolewa Jumatatu inaonesha kuwa mamilioni ya wasichana walio na umri mdogo wapo katika hatari ya kulazimishwa kuolewa ulimwenguni kote kutokana na janga la corona. "Familia yangu iliniambia sipaswi kukataa ombi kama hilo, kwani mvulana ambaye alitaka kunioa alitoka katika familia tajiri," Abeba mwenye umri wa miaka 14 aliambia BBC. Miezi michache tu iliyopita, alikuwa chini ya shinikizo kubwa kutoka kwa mama yake na ndugu zake kukubali mchumba, aolewe na kusaidia kupunguza shida za kifedha za familia yake wakati wa janga la Covid-19. Abeba anataka kuwa daktari lakini katika mji wake wa Gondar Kusini, nchini Ethiopia, elimu yake ya baadaye haina uhakika. Rabi, 16, bado anasoma shule ya upili huko Gusau, Nigeria, lakini marafiki zak...