Virusi vya corona: Je taifa la Tanzania linakabiliwa na mlipuko uliojificha?
Licha ya ushahidi kuonyesha kinyume, serikali ya Tanzania imeendelea kupuuzilia mbali athari ya virusi vya corona katika taifa hilo.
Hakuna takwimu rasmi
Hakuna takwimu za karibuni kuhusu vifo vinavyotokea Tanzania, na hakuna taarifa zozote zilizotolewa na serikali kuhusu athari za virusi vya rasmi tangu Mei mwaka jana, ambapo takriban visa 500 vya maambukizi vilikuwa vimeripotiwa na vifo 20 kufikia wakati huo.
Serikali imesisitiza kwamba hakuna haja ya kuwa na wasiwasi, na imekuwa ikiwachukulia hatua wale inaowatuhumu kwa kueneza "taarifa za uzushi".
CHANZO CHA PICHA,AFP
Maelezo ya picha,Rais Magufuli amekataa kutekeleza mpango wa chanjo na badala yake amekuza utumizi wa dawa za kitamaduni
Tulipowasiliana na naibu waziri wa afya Go...