Sylvestre Ilunga Ilukamba atakiwa kujiuzulu ndani ya saa 24
Wabunge nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamepiga kura kumuondoa madarakani Waziri Mkuu Sylvestre Ilunga Ilukamba
Bwana Ilukamba, ambaye hakuwepo wakati wa kura ya kutokuwa na imani naye iliyopigwa bungeni, amepewa saa 24 kujiuzulu.
Wabunge wanamshutumu Bw. Ilukamba, mshirika wa rais wa zamani Joseph Kabila, na mawaziri wake kwa utendaji kazi mbovu.
Kuanguka kwa serikali kunafungua milango kwa Rais Félix Tshisekedi kuteua mawaziri watiifu kwake.
Mweezi uliopita, Rais Tshisekedi aliuvunja muungano ulioundwa na mtangulizi wake, umoja ambao mawaziri washirika wake walitawala kwenye baraza la mawaziri.
Tangu wakati huo, Bw. Tshisekedi amekuwa akiwashawishi wabunge kuachana na muungano wa Bw Kabila, ambao hapo awali ulishikilia wengi bungeni, u...