Urusi na Iran: Uhusiano mgumu kati ya wapinzani wawili wa kihistoria ambao wanaungana kukabiliana na Magharibi
Urusi imesalia kuwa kisiwa baada ya kutengwa na mataifa mengi duniani baada ya uvamizi wake wa Ukraine, Hali ambayo ilifanya taifa hilo kutafuta miungano ya mataifa mengine ambayo katika nyakati zale bora zaidi isingezingatia: moja wapo ni uhusiano wake mgumu na Irani.
Ni mataifa yaliyogawanyika kwa masuala kadhaa, kuanzia kihistoria, kutokana na dhuluma ambayo Wairani wengi wanakumbuka kuwa waliteseka kutoka kwa Dola ya Urusi na Umoja wa Kisovieti, hadi kiuchumi, kwa vile wao ni wapinzani katika masuala ya nishati.
Lakini uadui wao na nchi za Magharibi mara nyingi huwaleta pamoja
Tangu aanzishe uvamizi wake nchini Ukraine, Rais wa Urusi Vladimir Putin amefanya safari tano nje ya nchi, zote zikipakana na mataifa ya zamani ya "stan" ya Soviet, isipokuwa safari yake ...