Thursday, November 14

Kimataifa

China yaipiku Marekani na kuchukua nafasi ya kwanza kama kivutio cha uwekezaji wa kigeni duniani
Kimataifa

China yaipiku Marekani na kuchukua nafasi ya kwanza kama kivutio cha uwekezaji wa kigeni duniani

Nusu ya uwekezaji mpya nchini Marekani kutoka katika makampuni ya kigeni ulishuka mwaka uliopita hatua iliosababisha taifa hilo kupoteza nafasi yake ya kwanza. Kwa upande mwingine, takwimu hizo zinaonyesha uwekezaji wa moja kwa moja katika kampuni za Wachina uliongezeka kwa asilimia 4 , na kulifanya taifa hilo kuchukua nafasi ya kwanza duniani. Kupanda kwa China kunaonesha ushawishi wake katika sekta ya kiuchumi duniani. China ilijipatia kipato cha $163bn (£119bn) mwaka uliopita , ikilinganishwa na $134bn zilizoingia Marekani, Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Biashara na Maenedeleo (UNCTAD) ulisema katika ripoti yake. Mwaka 2019, Marekani ilipokea $251bn kupitia uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni huku China ikijipatia$140bn. Huku China ikiwa kat...
Takribani viza 50,000 hutolewa na Marekani kwa bahati nasibu kila mwaka.
Kimataifa

Takribani viza 50,000 hutolewa na Marekani kwa bahati nasibu kila mwaka.

Rais mpya wa Marekani Joe Biden amewaondolea raia wa Tanzania vikwazo vya kushiriki bahati nasibu ya viza, mwaka mmoja baada ya kutangazwa kwa vikwazo hivyo. Januari 30, 2020 serikali ya Donald Trump ilitangaza kuwawekea Watanzania vikwazo vya kushiriki bahati nasibu hiyo pamoja na raia wa nchi nyingine kadhaa. Kwa mujibu wa afisa mmoja mwandamizi wa utawala uliopita wa Trump, nchi hizo ziliwekewa marufuku hiyo kwa kushindwa kufikia "kiwango stahiki cha ulinzi na kupashana taarifa". "Nchi hizi, kwa sehemu kubwa, zinataka kutoa msaada lakini kwa sababu mbali mbali zimefeli kufikia viwango vya chini tulivyoviweka," aliyekuwa Naibu Waziri wa Usalama wa Ndani wa Marekani Chad Wolf aliwaambia wanahabari baada ya kutangazwa kwa vikwazo. Hii leo, Ubalozi wa Marekan...
Virusi vya Corona: Uingereza yapiga marufuku abiria kutoka Tanzania,DRC
Kimataifa

Virusi vya Corona: Uingereza yapiga marufuku abiria kutoka Tanzania,DRC

Uingereza yapiga marufuku abiria kutoka Tanzania na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuzuia maambukizi ya aina mpya ya virusi vya corona. "Abiria wote kutoka Tanzania na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo hawataruhusiwa kuingia nchini Uingereza na katika mataifa ya Irish kuanzia saa kumi alfajiri," amesema Grant Shapps, waziri wa usafirishaji nchini Uingereza. Kuanzia tarehe 22 Januari, saa kumi alfajiri wasafiri wote kutoka au wamepita nchini Tanzania ndani ya siku 10 hawataruhusiwi kuingia Uingereza na mataifa ya Irish, na wale ambao wana haki ya makazi nchini Uingereza na wanatoka Tanzania watahitaji kujitenga nyumbani kwao watakapowasili. Katika masharti mapya nchini Uingereza dhidi ya Corona, lazima watu wabaki nyumbani au kutosafiri, pamoja na kutosafiri nje ya nchi labd...
Rais Joe Biden awaondolea Watanzania vikwazo kushiriki viza ya bahati nasibu
Kimataifa

Rais Joe Biden awaondolea Watanzania vikwazo kushiriki viza ya bahati nasibu

CHANZO CHA PICHA,REUTERS Maelezo ya picha,Takribani viza 50,000 hutolewa na Marekani kwa bahati nasibu kila mwaka. Rais mpya wa Marekani Joe Biden amewaondolea raia wa Tanzania vikwazo vya kushiriki bahati nasibu ya viza, mwaka mmoja baada ya kutangazwa kwa vikwazo hivyo. Januari 30, 2020 serikali ya Donald Trump ilitangaza kuwawekea Watanzania vikwazo vya kushiriki bahati nasibu hiyo pamoja na raia wa nchi nyingine kadhaa. Kwa mujibu wa afisa mmoja mwandamizi wa utawala uliopita wa Trump, nchi hizo ziliwekewa marufuku hiyo kwa kushindwa kufikia "kiwango stahiki cha ulinzi na kupashana taarifa". "Nchi hizi, kwa sehemu kubwa, zinataka kutoa msaada lakini kwa sababu mbali mbali zimefeli kufikia viwango vya chini tulivyoviweka," ali...
Kuapishwa kwa Joe Biden: Mfahamu Kamala Harris mwanamke mweusi atakayekuwa makamu wa rais wa Joe Biden
Kimataifa, Siasa

Kuapishwa kwa Joe Biden: Mfahamu Kamala Harris mwanamke mweusi atakayekuwa makamu wa rais wa Joe Biden

Bi Harris mwenye umri wa miaka 55, aliondoka kwenye kinyang'anyiro cha kuwania urais mwezi Disemba baada ya kutofanikiwa kushinda katika mchuano wa uteuzi wa kiti cha urais wa chama cha Democratic. Akikabiliana mara kwa mara na Bwana Biden wakati wa midahalo ya uchaguzi za awali , ambapo alikosoa jinsi Biden alivyosifu mahusiano ya ''kiraia'' ya kikazi aliyokuwa nayo na seneta wa zamani ambaye alipendelea ubaguzi wa rangi. Kamala alizaliwa katika Oakland, California, na wazazi wahamiaji :Mama yake alikua ni muhindi na baba yake Mjamaica. Alisoma hadi Chuo Kikuu cha Howard , ambacho ni moja ya vyuo maarufu walivyosomea watu weusi kihistoria. Alielezea muda wake chuoni hapo kama moja ya maeneo yaliyojenga maisha yake. Uchambuzi Wakati mwingine uteuzi unaotarajiwa ni kwa ajili ya sabab...