Thursday, November 14

Kimataifa

Biden aanza kazi kwa kutengua sera za Trump
Kimataifa, Siasa

Biden aanza kazi kwa kutengua sera za Trump

Rais mpya wa Marekani Joe Biden ameanza kutengua sera kadhaa muhimu za Donald Trump, saa chache baada ya kuapishwa. Rais Biden tayari amesaini maagizo ya watendaji 15 yanayolenga kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona. Amri nyingine ni kubadilisha msimamo wa utawala wa Trump juu ya mabadiliko ya hali ya hewa na uhamiaji. Biden ameanza kufanya kazi katika Ofisi ya Oval baada ya kuapishwa mapema Jumatano kama rais wa 46 wa Marekani. Kuapishwa kwa Biden kulikua na utofauti na nyakati nyingine yoyote kutokana na vizuizi vya maambukizi ya corona, na wachache walikuwepo kushuhudia viapo na sherehe. Donald Trump - ambaye bado hajakubali rasmi urais kwa Biden alikataa kuhudhuria hafla badala yake alikua na sherehe zake binafsi katika makazi yake. Biden ameapa kuwa ...
Waridi wa BBC: Maisha ya Alice Booth yalivyobadilika baada ya kukutana na mume wake mtandaoni
Kimataifa

Waridi wa BBC: Maisha ya Alice Booth yalivyobadilika baada ya kukutana na mume wake mtandaoni

Anne Ngugi BBC Swahili Maisha ya Bi. Alice Booth yamegeuka kuwa ya ajabu kila siku inayoitwa leo. Bi Alice anasema kila anapofikiria maisha yake ya nyuma anashangaa ni vipi ameweza kupiga hatua chanya baada ya matukio mawili mazito kutokea katika maisha yake. Tukio la kwanza lilikuwa ni kumpoteza mume wake wa kwanza na baadaye akaugua saratani. Lakini bila kutarajia, alipata mpenzi mwingine ambaye wameweza kujaliwa mtoto licha ya umri wake kuwa mkubwa. Awali madaktari walimwambia si rahisi kushika kwa yeye kushika mimba tena. Maisha yalivyogeua kuwa machungu Alice alikutana na mume wake wa kwanza aliyejulikana kwa jina la utani kama Gee wakiwa katika chuo kikuu cha Kenyatta nchini Kenya. "Katika ndoa yangu ya kwanza, tulijaliwa watoto watatu, wawili wa kike...
Kuapishwa kwa Joe Biden: Jinsi rais wa Marekani anavyotazamiwa kufuta nyayo za Trump Afrika
Kimataifa

Kuapishwa kwa Joe Biden: Jinsi rais wa Marekani anavyotazamiwa kufuta nyayo za Trump Afrika

Mohammed AbdulRahman Mchambuzi Saa 6 zilizopita Dunia inasubiri kushuhudia tukio kubwa katika siasa za Marekani. Ni kuapishwa mdemokrat Joe Biden kuwa Rais wa 46 wa taifa hilo kubwa . Tukio hilo pia litamaliza kipindi cha utawala wa miaka minne cha mrepublican Donald Trump, kilichokua na utata na mtikisiko katika siasa za kimataifa. Wakati huo huo baada ya kupewa mgongo na Trump bara la Afrika litarajie nini kutokana na utawala wa Biden na makamu wake Kamala Harris? Afrika lilianza kupewa kipaumbele na Marekani mnamo miaka ya 1960, wakati mataifa kadhaa yalipoanza kujinasua na ukoloni na kuanza kujipatia uhuru. Lakini sera za uhusiano huo zilitofautiana kwa kutegemea utawala gani uko madarakani, wa Warepublican au Wademokrats. Marekani ilitoa nafasi nyingi za elimu ya ...