Makamo wa Pili awajia juu wakandarasi ZRB na ZBC.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdalla, amewaonya wakandarasi wanaojenga jingo la Ofisi za ZRB Gombani na Ofisi za ZBC TV Mkoroshoni, kuacha tabia ya kutafuta sababu ya kwamba mvua ndio kigezo kilichopeleka kuchelewa kwa majengo hayo kumalizika kwa wakati.
Alisema tabia hiyo ya wakandarasi wanapopewa kazi za ujenzi kwa majengo ya serikali mwisho wake umefika, bali wanapaswa kujega kulingana na mikataba ya ujenzi waliosainiana na wenyeji wao.
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdalla, alitoa kauli hiyo baada ya kutembelea majengo hayo kwa nyakati tafauti, katika mwendelezo wa Ziara yake Kisiwani Pemba.
Akizungumzia jingo la Ofisi za ZRB Gombani, alimtaka mkandarasi huyo kuhakikisha jingo hilo analimaliza ndani ya muda uliopangwa, wakati...