Saturday, October 19

Kitaifa

Jamii yatambuweni maradhi yasiyopewa kipaumbele.
Kitaifa

Jamii yatambuweni maradhi yasiyopewa kipaumbele.

  NA MARYAM SALUM, PEMBA. JAMII Kisiwani Pemba imetakiwa kutambua yapo maradhi yasiyopewa kipaombele, ambayo yanaweza kumpata kila mtu na kila rika, hivyo ni vyema kuchukua tahadhari, katika kujikinga na maradhi hayo. Hayo yalielezwa na Mratibu wa kitengo cha maradhi yasiyopewa kipaombele Kisiwani Pemba, Dk Saleh Juma Mohamed wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi Ofisini kwake Mkoroshoni Chake Chake. Alisema wananchi waliowengi hufikiria kwamba maradhi hayo huwapata watoto wadogo tu, jambo ambalo sio sahihi kwani maradhi hayo huwapata watu wa rika lolote. “Watoto wadogo ndio wanaonekana kupatwa na maradhi ya mripuko, kwa sababu ndio ambao wanaonekana mara nyingi kucheza ama kuzurura ovyo, kwenye mazingira yasiyokuwa salama juu ya afya zao,” alisem...
WANAFUNZI wa Chuo cha Utawala wa Umma (IPA) tawi la Pemba, waishauri Ofisi ya mwanasheria mkuu wa Serikali Zanzibar
Kitaifa

WANAFUNZI wa Chuo cha Utawala wa Umma (IPA) tawi la Pemba, waishauri Ofisi ya mwanasheria mkuu wa Serikali Zanzibar

  WANAFUNZI wa Chuo cha Utawala wa Umma (IPA) tawi la Pemba, wameishauri Ofisi ya mwanasheria mkuu wa Serikali Zanzibar kuendelea kutoa elimu ya sheria kwa jamii, ili iweze kufahamu haki zao na namna ya umiliki na matumizi ya ardhi. Walisema, kumekua kukijitokeza migogoro mingi mitaani ambapo baadhi ya watu hujimilikisha ardhi kinyume na sheria, lakini kuwepo kwa sheria hiyo kutawezesha kutatua changamoto hiyo kwa kiasi kikubwa. Waliyasema hayo, wakati walipokua akizungumza na mwandishi wa habari mara baada ya kupatiwa mafunzo ya elimu ya sheria huko katika ukumbi wa chuo hicho mjini Chake chake. Kwa upande wake, mwanafunzi katika ngazi ya Diploma Juma Suleiman Hamad, alisema elimu ya sheria inahitajika kwa jamii kwani bado haina uwelewa kuhusiana na sheria ya umiliki ...
Wanafunzi wahimizwa kuendeleza usafi wa mazingira katika maeneo wanayoishi.
Kitaifa

Wanafunzi wahimizwa kuendeleza usafi wa mazingira katika maeneo wanayoishi.

  HABIBA ZARALI,PEMBA WANAFUNZI wa skuli mbalimbali zilizojiunga na klabu inayojishughulisha na mazingira Kisiwani Pemba ‘Roots And Shoots’ wametakiwa kutojisahau na badala yake waendeleze kuhifadhi usafi wa mazingira katika maeneo wanayoishi, ili kunusuru kutokea kwa maradhi mbalimbali ya mripuko. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Kisiwani humo Mratibu wa Kanda wa klabu hiyo Zanzibar Ali Juma Ali, alisema usafi wa mazingira ni moja kati ya njia inayoweza kuondosha maradhi ya mripuko yakiwemo ya kuharisha na kipindupindu, ambayo ni hatari kwa maisha ya binadamu. Alisema ni vyema usafi wa mazingira wanaoufanywa katika skuli zao wauendeleze katika maeneo yao yaliyowazunguka, ili kuweza kwenda sambamba na lengo la klub hiyo la utunzaji wa mazingira na kuleta afya nj...
Jamii itambue umuhimu wa kuwafahamisha  watoto kujikinga na maradhi ya mripuko.
Kitaifa, Wanawake & Watoto

Jamii itambue umuhimu wa kuwafahamisha watoto kujikinga na maradhi ya mripuko.

  HABIBA ZARALI,PEMBA. JAMII kisiwani Pemba imetakiwa kutambuwa umuhimu wa kuwafahamisha watoto wao, jinsi ya kujikinga na maradhi ya mripuko hasa katika kipindi hichi cha mvua kinachoendelea. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi  kwa nyakati tofauti wazazi na walezi kisiwani hapa, walisema katika maisha ya kila siku, ni vyema wazazi kuanzisha wigo wa mashirikiano katika malezi bora, ili watoto waweze kutambua na kutekeleza mambo mema yenye maslahi kwa maisha yao. Walisema kuwahimiza watoto kujuwa umuhimu wa afya  njema na kujikinga ma maradhi si ya madaktari peke yao, badala yake hata wazazi wana nafasi hiyo ambayo ni moja kati ya njia za kuwafikisha pahala pazuri katika maisha yao ya kila siku. Salma Suleiman  mkaazi wa Mkoani, alisema kutokana na athari kubwa...
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Uchumi na Uwekezaji, Mhe Mudrick Ramadhan Soraga anena.
Kitaifa

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Uchumi na Uwekezaji, Mhe Mudrick Ramadhan Soraga anena.

  Na Mwandishi wetu   WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Uchumi na Uwekezaji, Mhe Mudrick Ramadhan Soraga amesema kuwa hatokuwa tayari kutumbuliwa kwa makosa ya uzembe yatakayofanywa na wasaidizi wake. Kauli hiyo ameitowa katika kikao cha pamoja cha watendaji wa wizara yake kilichofanyika Mwanakwerekwe mkoa wa Mjini Magharibi Unguja. Alisema kuwa wanaingia katika Serikali ya awamu ya nane kwa kila Mtendaji atambuwe majukumu yake, ili kuendana na Kasi ya Rais wao. Hivyo awe Mkurugenzi, Katibu Hata msaidizi ambae atakuwa haendani na Kasi hiyo hatomuonea haya na badala yake atamuandikia barua ya kuomba kuondolewa ili awapishe wenzake wanaoendana na kasi hiyo. Sambamba na hiyo aliwataka watendaji hao kila mmoja atimize wajibu wake ili kuweza kufanikisha malengo y...