Saturday, October 19

Kitaifa

Dk. Hussein Ali Mwinyi ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Afya katika Wizara ya Afya na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja.
Kitaifa

Dk. Hussein Ali Mwinyi ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Afya katika Wizara ya Afya na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja.

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Afya katika Wizara ya Afya Dk. Jamala Adam Talib na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Dk. Ali Salum Ali. Kutenguliwa kwa uteuzi wa viongozi hao kunatokana na ziara aliyoifanya Rais Dk. Hussein leo (Novemba 18,2020) katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja kwa azma ya kujionea mwenyewe hali ya utoaji wa huduma na changamoto zinazoikabili Hospitali hiyo. Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee utenguaji huo unafuatia ziara hiyo aliyoifanya Rais Dk. Hussein na kupelekea kutenguliwa kwa viongozi hao kuanzia leo tarehe 18 Novemba, 2020 na kueleza kwamba watapangiwa kazi nyengine k...
Wadaiwa sugu wa Madeni ya Serikali kuwasilishwa kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Kitaifa, Sheria

Wadaiwa sugu wa Madeni ya Serikali kuwasilishwa kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdalla ameuagiza Uongozi wa Bodi ya Mapato Zanzibar {ZRB}kuwasilishwa Afisini kwake Ripoti ya Majina ya Wadaiwa sugu wote wa Madeni ya Serikali ndani ya Siku saba ili hatua za kisheria zichukuliwe mara moja dhidi ya wahusika hao. Alisema wapo baadhi ya Wafanyabishara na Wawekezaji wenye tabia ya kutumia migongo ya Wakubwa kukwepa kulipa Kodi kwa mujibu wa Sheria na Taratibu zilizowekwa jambo ambalo huviza ukusanyaji wa Mapato yanayohitajika kuendesha Serikali. Mheshimiwa Hemed Suleimna Abdalla alitoa agizo hilo alipofanya ziara fupi hapo Makao Makuu ya Bodi ya Mapato Zanzibar yaliyopo Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar kuangalia utendaji kazi wa Taasisi hiyo ya  Fedha. Alisema Bodi ya Mapato Zanzibar ndio tegemeo kubw...
Wazazi na Walezi kuweni   karibu na  watoto wenu ili wanapofikwa na vitendo vya udhalilishaji waweze kuwaeleza.
Kitaifa, Sheria, Wanawake & Watoto

Wazazi na Walezi kuweni karibu na watoto wenu ili wanapofikwa na vitendo vya udhalilishaji waweze kuwaeleza.

  Na Mwashungi Tahir   Imeelezwa  kwamba Wazazi na Walezi wametakiwa kuwa karibu na  watoto wao ili wanapofikwa na vitendo vya udhalilishaji waweze kuwaeleza baada ya kuonekana vitendo hivyo vinaongezeka Zanzibar kila siku. Hayo ameyasema Mkaguzi Msaidizi wa Polisi kutoka Makao Makuu ya Polisi Khamis Mwinyi Bakar   katika kikao na waandishi wa habari huko katika Ofisi ya Mtakwimu iliopo Mazizini wakati wa ikiwasilishwa  takwimu za Ukatili na Udhalilishaji wa Kijinsia  kwa wanawake na watoto. Amesema wazazi wengi wanakuwa na tabia ya kupuuza taarifa za awali za udhalilishaji ambazo wanapewa na watoto wao  jambo ambalo linapelekea vitendo hivyo kuzidi kukua zaidi hadi kuwaathiri.   “Tuwe na tabia ya kuwa karibu na watoto wetu ili kuwabaini kwa hara...
RAIS wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali hassan Mwinyi ameupongeza utayari wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli  wa kuahidi kuwa mstari wa mbele kumsaidia katika kutekeleza yale yote aliyoyaahidi wakati wa Kampeni.
Kitaifa, Siasa

RAIS wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali hassan Mwinyi ameupongeza utayari wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli wa kuahidi kuwa mstari wa mbele kumsaidia katika kutekeleza yale yote aliyoyaahidi wakati wa Kampeni.

  Rais Dk. Hussein Mwinyi aliasema hayo leo wakati akitoa salamu zake katika hafla ya kuapishwa kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa pamoja na Mawaziri akiwemo Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango, na Waziri wa Mmabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profsa Kabudi hafla iliyofanyika leo huko Chamwino, nje kidogo ya Jiji la Dodoma. Mapema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli aliwaapisha viongozi hao na baadae baadhi ya viongozi walipata nafasi ya kutoa salamu zao akiwemo Rais Dk. Hussein Mwinyi. Akitoa salamu zake hizo, Rais Dk. Hussein Mwinyi alieleza imani kubwa aliyonayo Rais Magufuli kwake hatua ambayo inaonesha matarajio ya wananchi kwa kiongozi wao huyo pamoja na Serikali yao ya Mapindu...