Saturday, October 19

Kitaifa

Mwili wa aliekuwa askari wa kikosi cha KVZ wapatikana pamoja na bunduki.
Kitaifa, Sheria

Mwili wa aliekuwa askari wa kikosi cha KVZ wapatikana pamoja na bunduki.

MWANDISHI WETU, PEMBA.     JESHI la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba limefanikiwa kuupata mwili wa aliekuwa askari wa kikosi cha KVZ Khalfan Junedi mwenye miaka 25 aliuwawa baada ya wiki tatu zilizopita huko eneo la Ngwachani Wilaya ya Mkoani. Pamoja na mwili huo pia lilifanikiwa kuipata bunduki aina ya AK47 katika eneo la Ngwachani Novemba 12 majira ya saa 2:00 usiku ambayo magazine yake ikiwa na risasi 21. Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Ahmed Khamis Makarani amesema  mwili huo ulipatika katika kijiji cha chonga kwenye bonde la Kisitu mbwa. Alisema kuwa, Novemba 15 walifanikiwa kuupata mwili wa askari huyo baada ya kumkamata mtu mmoja anaejulikana kwa jina la Ussi Foum Machano mkaazi wa Ngwachani, ambae aliwapeleka ...
SOS yatumia Milioni 6,391,000/= kuwapatia wanafunzi chakula.
Kitaifa

SOS yatumia Milioni 6,391,000/= kuwapatia wanafunzi chakula.

JUMLA ya shilingi Milioni 6,391,000/= zimetumiwa na SOS kwa ajili ya kununulia chakula, wanafunzi wanaokaa kambi katika skuli 10, ambazo wanafunzi wake wamo katika mpango wa kuimarisha familia unaosimamiwa na shirika hilo. Skuli hizo ambazo zimenufaika na chakula hicho ni pamoja na Vitongoji Msingi na Sekondari, Tumbe Msingi na Sekondari, Ngwachani Msingi na Maendeleo Sekondari, Mjawiri Msingi na Mjawiri Sekondari na Michenzani Msingi na Sekondari. Vyakula hivyo vilivyotolewa ni sukari kilo 150 zenye thamani ya shilingi 231,000/=, maharage kilo 600 yenye thamani ya shilingi 132,000/=, Mchele liko 2100 zenye thamani ya shilingi 294,000/=, sukari kilo 500 yenye thamani ya shilingi 830,000/=, Unga wa ngano kilo 500 wenye thamani ya shilingi 590,000/= na mafuta ya kula lita 200 yenye...
JET yampongeza Rais Magufuli.
Kitaifa

JET yampongeza Rais Magufuli.

  CHAMA Cha Waandishi wa Mazingira Tanzania (JET) kimempongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli, kwa kuchaguliwa tena kuiyongoza Tanzania katika kipindi chake cha pili cha miaka mitano. Kwamujibu wa Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa chama hicho Tanzania John Chikomo, Jijini Dar Esalaam kwa vyombo vya habari, imesema kuchaguliwa kwa Rais Magufuli kuiyongoza tena Tanzania ni ishar ya matumaini mema, na imani ya hali ya juu waliyonayo wananchi wa Tanzania kwake. Mkurugenzi huyo alisema Dk Magufuli akilihutubia Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliweza kuelezea vipaombele mbali mbali, ambavyo vinagusa moja kwa moja masuala ya Mazingira, kama juhudi za kuendeleza matumizi ya nishati Jadidifu nchini pamoja na sekta ya...
Kampuni ya Kimataifa ya Arena yenye Makao  Makuu yake Nchini Ujerumani imeonyesha nia ya kutaka kuwekeza  Visiwani Zanzibar
Kitaifa

Kampuni ya Kimataifa ya Arena yenye Makao Makuu yake Nchini Ujerumani imeonyesha nia ya kutaka kuwekeza Visiwani Zanzibar

  Na.Othman Khamis OMPR.     Uongozi wa Kampuni ya Kimataifa ya Arena yenye Makao Makao Makuu yake Nchini Ujerumani inayojishughulisha na Miradi ya Uwekezaji katika Sekta ya Nishati ya Umeme imeonyesha nia ya kutaka kuwekeza Miradi yake Visiwani Zanzibar baada ya kuridhika na mazingira mazuri yaliyopo ya Uwekezaji. Mwakilishi wa Kampuni hiyo Bwana Souheil Freich aliyeambatana na Uongozi wa Kampuni ya Flagfin yenye Makao Makuu yake Jijini Dar es salaam alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Hemed Suleiman Abdalla hapo Vuga Mjini Zanzibar. Bwana Souheil Freich alisema alikuwa akifuatilia harakati za Sera na Ilani za Uchaguzi Mkuu uliopita na kuridhika nazo kitendo kilichoipa ushawishi Kampuni yake kutaka kuitumi...
Wapongeza kasi ya DK. Mwinyi.
Kitaifa

Wapongeza kasi ya DK. Mwinyi.

  WANANCHI na Viongozi wa Serikali Kisiwani Pemba, wamepongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi, kwa kasi alioanza nayo katika kuingoza Zanzibar katika kipindi cha miaka mitano. Walisema kutokana na kasi aliyoanza nayo kwa kuteuwa viongozi vijana, akiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdalla, pamoja na kunza kwa ziara yake ya kwanza bandarini ni dhahiri kuwa awamu yake itakuwa ni uchapaji wa kazi kwa vitendo. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tafauti, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othaman alisema kwa kasi aliyoanza nayo DK.Mwinyi ni yakupongezwa, hivyo viongozi na wananchi kujipanga kwendana na kasi yake. Alisema vijana wanapaswa kumuunga mkono Rais wa Zanzibar na Mweny...