Wananchi kuchukua tahadhari juu ya Kichocho.
WANANCHI Kisiwani Pemba wametakiwa kuendelea kujitahidi kuchukua tahadhari juu ya maradhi ya Kichocho, katika kipindi hiki cha mvua za Vuli zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali.
Wito huo umetolwa na mratib wa kitengo cha Maradhi yasiopewa Kipau Mbele Pemba, Dk.Saleh Juma Mohamed huko Ofisini kwake mkoroshoni Chake Chake Pemba.
Dk.Saleh alisema katika kipindi hiki cha mvua za vuli zinazoendelea kunyesha, vizuri wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kubwa juu ya maradhi hayo, kwa kuacha kutumia maji katika madimbwi au kwenye mabwa badala yake kutumia maji ya mfereji kwa shuhuli zao mbali mbali.
Alisema maradhi ya kichocho ni miongoni mwa maradhi yanayo uwa kidogo kidogo kwani, baktiri wa maradhi hayo anayojulikana kwa jina la Bilharzia(Schistosomiasis) hushi katika m...