Saturday, October 19

Kitaifa

Wabunge wamemthibitisha mbunge wa jimbo la Ruangwa mkoani Lindi, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa kuwa Waziri Mkuu.
Kitaifa

Wabunge wamemthibitisha mbunge wa jimbo la Ruangwa mkoani Lindi, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa kuwa Waziri Mkuu.

  Na.Mwandishi Wetu Dodoma   SPIKA wa Bunge la 12 Job Ndugai amesema wabunge wamemthibitisha mbunge wa jimbo la Ruangwa mkoani Lindi, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa kuwa Waziri Mkuu kwa miaka mitano mingine (2020-2025) kwa kupata kura zote 350 zilizopigwa na wabunge sawa na asilimia 100. “Kura zote zilizopigwa ni 350 hakuna iliyoharibika, hakuna kura ya hapana. Kura zote 350 zimemthibitisha Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, kwa hiyo ndugu wabunge Mheshimiwa Majaliwa amethibitishwa na Bunge hili kuwa Waziri Mkuu kwa kura 350 sawa na asilimia 100.” Spika Ndugai ameyasema hayo leo (Alhamisi, Novemba 12, 2020) Bungeni jijini Dodoma baada ya kupokea jina la Waziri Mkuu lililowasilishwa bungeni na Mpambe wa Rais na kisha wabunge kupiga kura kwa ajili ya kulithibit...
SOS yakabidhi  chakula kwa wanafunzi.
Kitaifa

SOS yakabidhi chakula kwa wanafunzi.

SHIRIKA la SOS Kisiwani Pemba limekabidhi msaada wa chakula wenye thamani ya shilingi Milioni 1,616,000/=, kwa uongozi wa skuli ya Msingi na sekondari Vitongoji Wilaya ya Chake Chake, kwa ajili ya wanafunzi wanaoishi katika kambi maalumu ya kujiandaa na mitihani yao mwaka huu. Msaada huo kwa skuli ya Msingi Vitongoji ni Mchele kilo 200, sukari kilo 50, maharage kilo 60, unga wa ngano kilo 50, mafuta ya kupikia lita 20, sabuni ya kufulia kilo 15 na Rimu za box za karatasi box 3 vyote vikiwa na thamani ya shilingi laki 773,000/=. Kwa upande wa skuli ya Sekondari Vitongoji vitu walivyokabidhiwa ni mchele kilo 250, sukari kilo 50, maharage kilo 60, unga wa ngano kilo 50, mafuta ya kula lita 20, sabuni ya unga kilo 15 na Rim box tatu za Karatasi vitu vyote vikiwa na tahamani ya Sh...
Dk. Hussein Mwinyi  azindua  Baraza la Kumi la Wawakilishi
Kitaifa

Dk. Hussein Mwinyi azindua Baraza la Kumi la Wawakilishi

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali  Mwinyi amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Nane itawekeza kwenye michezo katika kuibua, kuelea na kuendeleza vipaji vya vijana. Rais Dk. Hussein Mwinyi aliyasema hayo leo katika hotuba yake ya uzinduzi wa Baraza la Kumi la Wawakilishi hafla iliyofanyika huko katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani, nje kidogo ya Jiji la Zanzibar. Katika hotuba yake hiyo, Rais Dk. Hussein Mwinyi alisema kuwa katika hatua hiyo ya kuekeza kwenye michezo itakwenda sambamba na kukaa na wadau wa soka kutafuta jawabu la kuamsha msisimko wa ligi ya Zanzibar. “Wakati nakua timu za Zanzibar za Small Simba, Malindi, Mlandege na KMKM zilikuwa ni timu zenye sifa na kuchachafya timu za Bara na zile z...
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdalla awaomba Viongozi na Watumishi wa Umma kujitambua.
Kitaifa

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdalla awaomba Viongozi na Watumishi wa Umma kujitambua.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdalla amewaomba Viongozi na Watumishi wa Umma wajitambue na kujitathmini katika utekelezaji wa majukumu yao waliopewa  na Taifa  ili ile kiu ya kuwatumikia Wananchi ifanikiwe vyema. Alisema baadhi ya Viongozi ama Watendaji watakaojihisi kwamba hawaendani na kasi ya Serikali iliyoanza kazi zake muda mfupi uliopita baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu ni vyema wakaondoka kwa Heshima katika maeneo yao ya kazi waliyokabidhiwa. Mhe. Hemed Suleiman Abdalla alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kupokewa ndani ya Ofisi yake Mpya kama Mtendaji Mkuu wa Serikali wakati akizungumza na Viongozi wa Idara na Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar hapo Vuga Mjini Zanzibar. Alisema hapendezi kuona ...
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi amuapisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Kitaifa

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi amuapisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Hussein Ali Mwinyiamemuapisha Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla kuwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar. Hafla hiyo ya kiapo imefanyika Ikulu Jijini Zanzibar ambayo ilihudhuriwa na  viongozi mbali mbali akiwemo Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othamn Mkungu, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee. Wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Dk. Mwinyi Talib Haji, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan KhatibMufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Naibu Kadhi Mkuuwa ZanzibarSheikh  Hassan Othman Ngwali, Naibu Mufti Mkuu Sheikh Mussa Wadi, Mku...