Saturday, October 19

Kitaifa

Makamu wa Pili wa Rais Mteule wa Zanzibar  Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdallah anena.
Kitaifa

Makamu wa Pili wa Rais Mteule wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdallah anena.

  Makamu wa Pili wa Rais Mteule wa Zanzibar  Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdallah alisema Wananchi wa Zanzibari wanapaswa kujenga matumaini makubwa kwa Serikali Mpya itakayojizatiti kuwajibika ipasavyo katika kuwaletea maendeleo. Alisema uwajibikaji huo utakaozingatia kutotoa nafasi kwa Watendaji wenye tabia ya kukumbatia dhambi, ubadhirifu, uzembe pamoja na wizi ndio mfumo utakaotumiwa na Serikali chini ya usimamizi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Hussein Ali Mwinyi. Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdallah alitoa kauli hiyo akizungumza na  Wanahabari muda mfupi baada ya kula kiapo cha Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kufuatia Uteuzi uliofanywa na Rais wa Zanzibar na hapo hapo Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mh. Zubeir Ali Maulid kuli...
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi afanya uteuzi wa  Makamo wa Pili wa Rais.
Kitaifa

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi afanya uteuzi wa Makamo wa Pili wa Rais.

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amemteua Hemed Suleiman Abdulla kuwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar.   Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee ilieleza kwamba  Rais Dk. Hussein Mwinyi amemteua Hemed Suleiman Abdulla kuwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu Namba 39 (1) na 39(2) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.   Kabla ya Uteuzi huo Hemed Suleiman Abdulla alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba.   Uteuzi huo umeanza leo tarehe 08 Novemba, 2020.   Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822   E-mail: rajabmkasaba@yaho...
Walimu Mkoani waipongeza UNESCO.
Kitaifa

Walimu Mkoani waipongeza UNESCO.

  WALIMU wa skuli za msingi na Sekondari Wilaya ya Mkoani Kisiwani Pemba, wamelipongeza shirika la Umoja wa Mataifa elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO)Tanzania, kuingiza wilaya ya mkoani katika wilaya nne za Tanzania katika mradi wa majaribio wa Stadi za Maisha, Ukimwi, afya ya Uzazi na Elimu ya Jinsia. Walimu hao wamesema kuwa hatua hiyo ya wilaya ya mkoani imekuwa na habati ya pakee, kunufaika na mafunzo hayo ambayo yatawasaidia kwa kiasi kikubwa katika ufundishaji wa wanafunzi maskuli. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, huko katika skuli ya Mohamed Juma Pindua Chokocho Wilaya ya Mkoani, mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya siku sita ya kuwajengea uwezo walimu 15 za wilaya hiyo. Mwalimu wa ushauri skuli ya Sekondari Mkanyageni Time Mohamed Shamuuni, alisema...
ZECO kufikisha umeme vijiji vipya Makoongwe.
Kitaifa

ZECO kufikisha umeme vijiji vipya Makoongwe.

  SHIRIKA la Umeme Zanzibar ZECO Tawi la Pemba, limewataka wananchi wa Kisiwa cha Makoongwe Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kuisni Pemba, ambao hawajapatiwa huduma ya umeme kuanza maandalizi ya kupokea huduma hiyo. Kauli hiyo imetolewa na Afisa Mipango na utafiti shirika la umeme Tawi la Pemba Ali Faki Ali, wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Makoongwe, kufuatia kukubalia ombi lao la kupatiwa umeme kwa njia ya mkopo kama ilivyokuwa kwa wenza wao mwaka 201/2015 ulipofikisha umeme kisiwani humo. Alifahamisha mwaka huo vijiji vyote vilivyomo ndani ya kisiwa hicho walipatia huduma hiyo, lakini sasa tayari kumeshakuwa na vijiji vipya vinavyohitaji huduma hiyo, huku watu 126 wapo tayari kwa hatua ya kwanza kupatiwa umeme huo. “Shirika limekubali ombo lenu mulilolitoa septem...
CFP na Mrajisi wakutana.
Kitaifa

CFP na Mrajisi wakutana.

  MRAJIS wa JUmuiya zisizo za Kiserikali Zanzibar Ahmed Khalid Abdalla, ameitaka Jumuiya ya community forest Pemba (CFP) Pemba kuhamasiaha vikundi vyengine juu ya suala zima la utunzaji wa mazingira kwa kuhakikisha wanapanda miti ya kutosha. Alisema iwapo kutakuwa na vikundi vingi na vikaweza kupanda miti ya kutosha ya mikandaa, katika maeneo ambayo yako wazi maji ya bahari hayotokua na nguvu kuja juu na kuharibu mashamba ya kilimo. Akizungumza na mwanidhsi wa habari hizi, mara baada ya kumalizika kwa kikao cha pamoja baina ya ofisi ya Mrajis wa NGOs Zanzibar na viongozi wa CFP, kikao kilichofanyika minyenyeni Gando Wilaya ya Wete mkoa wa Kaskazini Pemba. Alisema lazima wananchi wachukue juhudi katika kunusuru maeneo maji ya bahari kutokuvamia maeneo ya kilimo, pamoja ...