Wanasayansi washindwa kufumbua fumbo la uwepo wa dhahabu nyingi duniani.
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,
Mlipuko wa nyota kubwa angani huenda unachangia wingi wa dhahabu, lakini haitoshi
Kila uchao kiwango cha dhahabu ambayo haijachimbwa kinaendelea kupungua duniani.
Kiwango cha dhahabu ilichosalia duniani kinakadiriwa kuwa karibu tani 50,000, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na wanajiolojia wa Marekeni.
Tafiti zilizofanywa awali zilibaini kuwa dhahabu haiwezi kukuzwa upya.
Hata hivyo tafiti tofauti katika miaka ya hivi karibuni zimefichua kuwa kuna hifadhi kubwa ya dhahabu nje ya sayari ya dunia.
Inasadikiwa kuwa kiwango hicho kikubwa cha dhahabu ambacho sio ya kawaida imewafanya wanasayansi kukuna vichwa kwa miaka kadhaa wakijaribu kutafuta inapatikana wapi hasa.
Ripoti iliyotolewa wiki hii inaashiria kuwa kiwango c...