Friday, October 18

Kitaifa

PBZ Tawi la Wete imeadhimisha siku ya wateja.
Biashara, Kitaifa

PBZ Tawi la Wete imeadhimisha siku ya wateja.

  BENK ya watu wa Zanzibar PBZ Tawi la Wete, imeadhimisha siku ya wateja wa Benk, kwa kujumuika na wateja wao na kuwashukuru kwa kuendelea kuwa na imani na benk yao. Tawi hilo lenye maskani yake bopwe Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, imeadhimisha siku hiyo kwa ukataji wa keki na kujumuika na wateja wake. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, kaimu meneja wa benk hiyo Ahmed Abubakar Mohd, aliwashukuru wateja wa benk hiyo kwa kuendelea kuwa na imani na benk yao, na kuahidi kuwahudumikia kwa hali na mali. Alisema benk hiyo imekua ikitoa huduma mbali mbali kwa jamii, ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na zenye uhakika, kuhakikisha uchumi unakuwa na kufikia uchumi wa buluu. “Sisi leo tumeona tuungane na wananchi wetu katika kuadhimisha siku ya wateja wa mabenk...
Wajumbe wa kamati  washauriwa.
Kitaifa

Wajumbe wa kamati washauriwa.

WAJUMBE wa kamati za mashauriano za shehia kutoka Wilaya nne za Pemba, zimeombwa kuwa makini na kujifunza mambo mazuri kutoka katika kamati ambazo zimekua za mfano. Wajumbe wa kamati hizo wamekutana hivi karibuni, katika skuli ya msuka Sekondari Wilaya ya Micheweni kwa lengo la kuwasilisha mipango kazi yao ambayo wameitekeleza katika shehia zao na kutoa mafanikio. Akizungumza na waandishi wa habari Afisa Miradi kutoka Taasisi ya Milele Zanzibar Foundation, Fatma Khamis Silima alisema mashirikiano ni jambo zuri kwa viongozi wakamati hizo, katika kusaidiana pale ambapo kamati moja inapohitaji kujifunza kwa wenzake. Alisema zipo kamati zimefanya vizuri katika utekelezaji wa mipango kazi yake, ni vyema kwa kamati nyengine kujifunza huko ili kamati zote kuwa na mipango kazi bor...
Tuhuma za kutorosha na kubaka bado zamsotesha rumande.
Kitaifa, Sheria, Wanawake & Watoto

Tuhuma za kutorosha na kubaka bado zamsotesha rumande.

  Mtuhumiwa Bakar Mbwana Juma mwenye umri wa miaka 32 mkaazi wa Jomvu Kengeja anaekabiliwa na shitaka la Kumtorosha na Kumbaka msichana mwenye umri wa 17 ameiambia mahakama ya Mkoa Chake Chake kuwa yeye hahusiki na tukio hilo kwani muda uliotajwa kutenda kosa hilo alikua kwenye kibanda akinywa kahawa. Aliambia mahakama hiyo kuwa yeye ni mfanya kazi wa ujenzi wa nyumba hivyo anakawaida ya kurudi kazini  baina ya saa moja hadi saa moja na nusu za usiku na mara zote hufikia kwenye mkahawa kabla ya kwenda anakoishi. Alidai kuwa siku ambayo alituhumiwa kufanya tukio hilo alirudi kazini majira ya moja za usiku na kifikia mgahawani na kupata kahawa akiwa yeye na marafiki zake. Alifahamisha kuwa baada ya kunywa kahawa alirudi nyumbani na kuigia chooni kwa ajili kujiandaa na sa...
Mgombe uwakilishi Ole aahidi neema
Kitaifa, Siasa

Mgombe uwakilishi Ole aahidi neema

  MGOMBEA Uwakilishi wa jimbo la Ole kupitia chama cha Mapinduzi CCM, Wilaya ya Chake Chake Massoud Ali Mohameda, amewataka wananchi wa jimbo hilo kuhakikisha wanamchagua ili aweze kuwaletea maendeleo. Alisema iwapo watamchagua atakua ni mwakilishi wa wananchi wote, hivyo maendeleo ni ya watu wote kwani maendeleo hayachagui chama, dini, kabila wala rangi. Aliyaeleza hayo katika mkutano wa kampeni wa jimbo la Ole, wakati alipokua akiomba kura kwa wananchi wa jimbo hilo, kuelekea uchaguzi Mkuu wa Zanzibar. Aliwataka wazee na wanaole kuhakikisha hawapotezi bahati yao hiyo ambayo wameikosa kwa muda mferu, hivyo wanapaswa kumchagua ili kuwatumikia wanaleo. Mgombea huyo alisema ndani ya ilani ya CCM ya 2020/2015 wananchi wa jibo la ole, vimo vipaombele vingi vinawagusa ka...
Wawi kutekeleza ilani kwa Vitendo.
Kitaifa, Siasa

Wawi kutekeleza ilani kwa Vitendo.

  MGOMBEA Uwakilishi wa jimbo la Wawi Wilaya ya Chake Chake, kupitia chama cha Mapinduzi CCM, Bakari Hamad Bakari amesema iwapo wananchi wa jimbo hilo watamchagua atahakikisha wananchi wote wanakuwa kitu kimoja katika kuleta maendeleo ya jimbo hilo. Alisema maendeleo ya jimbo la wawi yataletwa na wananchi wajimbo hilo, iwapo watakuwa pamoja na viongozi wao waliowachangu kupitia chama cha Mapinduzi, kwani ndio wanaojuwa shida za wananchi hao. Mgombea huyo aliyaeleza hao wakati katika mkutano wa kampeni za chama hicho, huko Matungu Wadi ya kibokoni jimbo la Wawi Wilaya ya Chake Chake. Alisema ilani ya CCM 2020/2025 ibara ya 136 (c) imeahidi kuzalisha ajira kwa vijana zipatazo 300,000 kwenye sekta rasmi na isiyo rasmi ifikapo 2025, ambapo zikigaiwa kwa majimbo ya Zanzibar...