Friday, October 18

Kitaifa

VIDEO: Mama  Maryam  Mwinyi amuombea kura DK. Hussein Ali Mwinyi.
Kitaifa, Siasa

VIDEO: Mama Maryam Mwinyi amuombea kura DK. Hussein Ali Mwinyi.

  Waswahili wanasema Mwanamme yeyote Yule ambaye amepiga hatua ya mafanikio basi ujue kuwa nyuma yake kuna mwanamke ambae amesaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha kwa upatikanaji wa mafanikio hayo. Mama  Maryam  Mwinyi Mke wa Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi na yeye kwa upande wake anataka kuthibisha ukweli wa msemo huo kwani wakati wote hatua kwa hatua yuko sambamba na Dr. Hussein Mwinyi katika kuusaka Urais wa Zanzibar kupia tiket ya Chama cha Mapinduzi. Huko Katika kijiji cha Shumba Mjini Mama Maryam  alikutana na akina mama wa shehia hio ambapo bila ya ajizi aliwaomba akina  mama hao kumchagua Dr. Hussein Ali Mwinyi pamoja na wagombea wengine kupitia chama cha Mapinduzi ili waweze kupata ridhaa ya kuiongoza  Zanzibar kwa kipindi cha miaka mitanoi jayo kwa leng...
Rushwa muhali bado ni tatizo kukomesha vitendo vya udhalilishaji.
Kitaifa, Sheria, Wanawake & Watoto

Rushwa muhali bado ni tatizo kukomesha vitendo vya udhalilishaji.

Licha ya juhudi mbali mbali zinazochukuliwa na Serikali pamoja na Asasi za kiraia kuielimisha Jamii madhara ya Udhalilishaji wa kijinsia kwa Watoto  na jinsi ya kutoa ushahidi kwa kesi hizo lakini bado inaonekana matendo hayo  yanaendelea kujitokeza  kutokana na Muhali uliopo kwa Wanajamii. Hayo yamesema na wajumbe wa Mtandao wa  kupinga Udhalilishaji kutoka Wilaya ya Mkoani  katika kikao  cha uwasilishaji wa ripoti za utekelezaji wa majukumu yao ya kutoa Elimu  juu ya madhara ya Udhalilishaji wa Kijinsia kwa Jamii huko ukumbi wa Chama cha Wandishi wa habari Wanawake Tanzania Zanzibar  [ Tamwma]  Mkanjuni Chake chake Pemba. Wanajamii hao. Wamesema Jamii inaonekana kuyafumbia macho na kuyafanyia suluhu Mitaani matendo ya udhalilishaji jambo ambalo linasababisha kuongezeka sikuhadi...
Dk. Hussein Ali Mwinyi:  kama nikipata ridhaa ya kuwa rais wa Zanzibar, nitahakikisha kunatungwa sheria, ambayo itawawezesha wajane kupata haki zao stahili.
Biashara, Kitaifa, Sheria, Siasa, Wanawake & Watoto

Dk. Hussein Ali Mwinyi: kama nikipata ridhaa ya kuwa rais wa Zanzibar, nitahakikisha kunatungwa sheria, ambayo itawawezesha wajane kupata haki zao stahili.

NA MWANDISHI WETU, PEMBA .   MGOMBEA urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi ‘CCM’ Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema kama akipata ridhaa ya kuwa rais wa Zanzibar, atahakikisha kunatungwa sheria, ambayo itawawezesha wajane kupata haki zao stahili, kama yalivyo makundi mengine. Alisema anaelewa changamoto kadhaa zinazowakumba wanawake hao, iwe kwa wale wanaoachwa au kufiwa na waume, kwa kukoseshwa haki zao na kutupiwa mzigo wa malezi na huduma kwa watoto. Mgombea huyo wa urais, aliyasema hayo ukumbi wa zamani wa baraza la Wawakilishi mjini Wete Pemba, alipokuza akizungumza na wanachama wa jumuiya ya wajane Zanzibar kwa upande wa Pemba. Alisema, anatambua kuwa Zanzibar lipo kundi kubwa la wajane ambalo linaendelea kuteseka na kuhangaika huku na kule na wale wanaume w...
DK. Shein afungua jengo jipya la abiria na eneo la maegesho ya ndege.
Kitaifa

DK. Shein afungua jengo jipya la abiria na eneo la maegesho ya ndege.

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa na miundombinu bora ya kisasa ya usafiri ni nyenzo muhimu katika kuimarisha uchumi wa ndani ya nchi kupitia vyanzo vya ndani na nje ya nchi.   Dk. Shein aliyasema hayo leo katika ufunguzi wa jengo jipya la abiria na eneo la maegesho ya ndege katika kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume (Terminal III), lililopo Kiembesamaki Unguja ambapo viongozi kadhaa walihudhuria akiwemo Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ambaye pia, ni Mgombea wa Urais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi na viongozi wengine  na wananchi. Katika maelezo yake, Rais Dk. Shein alisema kuwa na kiwanja cha ndege kikubwa na cha kisasa ni...
ADC yalaani vitendo vya uvunjifu wa amani.
Kitaifa, Siasa

ADC yalaani vitendo vya uvunjifu wa amani.

CHAMA cha Alliance For Democratic Change (ADC), kimelaani vikali kauli zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa, ambazo zinaashiria uvunjifu wa amani nchini, huku wakivitaka vyombo vya ulinzi na usalama na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania Jaji Mutungi kutokuvifumbia macho na kuvipuuza. Chama hicho kimesema kauli hizo za chokochoko hata mwaka 2001, zilikuwa zikitolewa na baadhi ya viongozi wa siasa wakati wa kampeni, jambo ambalo mwisho wake zilipelekea vurugu na kusababisha taifa kuingia doa. Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa ADC Taifa, Omar Costantino Pweza wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali vya habari, huko katika ofisi ya Kanda ya ADC Wawi, kufuatia kujitokeza kwa viashiria vya uvunjifu wa amani Kisiwani Pemba. Mk...

Warning: file_get_contents(): http:// wrapper is disabled in the server configuration by allow_url_fopen=0 in /data/40/5/71/99/5397425/user/6768456/htdocs/portal/wp-content/plugins/xt-visitor-counter/xt-visitor-counter.php on line 48

Warning: file_get_contents(http://api.xtrsyz.org/xt-visitor-counter/default.php?domain=www.pembapress.club&time=1729261881): failed to open stream: no suitable wrapper could be found in /data/40/5/71/99/5397425/user/6768456/htdocs/portal/wp-content/plugins/xt-visitor-counter/xt-visitor-counter.php on line 48