Friday, October 18

Kitaifa

Dk. Hussein Ali Mwinyi :Nitasimamia uwajibikaji na watakoshindwa nitawawajibisha.
Kitaifa, Siasa

Dk. Hussein Ali Mwinyi :Nitasimamia uwajibikaji na watakoshindwa nitawawajibisha.

NA HAJI NASSOR, PEMBA     NGOMBEA urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema iwapo wananchi wa Zanzibar watampa ridhaa ya kushika nafasi hiyo, atahakikisha, anasimamia uwajibikaji na watakoshindwa atawawajibisha, ili mafanikio ya kweli yapatikane. Alisema, hayo ndio kipaumbele chake cha kwanza mara atapomaliza kuapishwa, kwani mambo hayo ni miongoni mwa yanadhoofisha kwa kiasi kikubwa maendeleo ya jamii. Mgombea huyo wa urais, aliyasema hayo Jimbo la Gando wilaya Wete mkoa wa kaskazini Pemba, alipokuwa akizugumza na mamia ya wanaccm na wananchi wengine, kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni wa chama hicho. Alisema kuwa, serikali atakayoiongoza hatopenda hata kidogo kuona ndani yake, mna watendaji wasiopenda...
Kitaifa, Siasa

VIDEO: Wagombea CCM jimbo la Pandani nao wanadi sera zao.

Mjumbe wa Halmashauri kuu  ya CCM Taifa Ramadhan Shaib Juma amewataka wana CCM na wananchi wote wapenda amani kuwachagua wagombea wa Chama cha Mapinduzi na  kujitokeza kuendelea kuomba kura kwa wananchi wote bila ya kujali  itikadi za kisiasa, kwani  sera za CCM zinaelekeza  kuleta maendeleo kwa wananchi wote. Ndugu Ramadhan amesema hayo wakati alipokuwa akizungumza na wana CCM pamoja na wananchi wa Jimbo la Pandani katika Mkutano wa kampeni wa Jimbo hilo huko shengejuu wakati wa kuwanadi wagombea wa nafasi ya Uwakilishi, ubunge pamoja na madiwani. Kwa upande wake Mgombea wa Uwakilishi wa Jimbo la Pandani ndugu Khamis Dadi Khamis amewaomba wana CCM wote na wapenda maendeleo kumchagua yeye pamoja na wagombea wote wa CCM wa Jimbo hilo ili waweze kuunganisha nguvu zao katika kukuza maen...
NRA, Kupandisha mishahara kwa walimu.
Kitaifa, Siasa

NRA, Kupandisha mishahara kwa walimu.

  MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia chama cha NRA Khamis Faki Mgau, amesema iwapo wananchi wa Zanzibar wakachagua kuongoza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, atahakikisha anapandisha mshara wa walimu kima cha chini kuanzia laki nane (800,000/=), pamoja na vikosi vya SMZ kupokea mshahara sawa na askari wa JWT kwani kazi zao za ulinzi zinafanana. Mgombea huyo aliyaeleza hayo huko katika uwanja wa kangagani, wakati wa uzinduzi wa kampenzi za chama hicho Kisiwani Pemba, pamoja na kuwanadi wagombea ubunge, uwakilishi na udiwani kupitia NRA. Alisema mambo hayo yanawezekana iwapo chama hicho kitapatiwa ridhaa ya kuongoza Zanzibar, kwani atahakikisha walimu na vikosi vya ulinzi vinabadilika mishahara yao kutokana na kazi wanazozifanya kwenye nchi. “Nduguzangu wa kangagani, hii...
Milele yakabidhi vifaa kwa Hospitali ya Chake Chake.
Kitaifa

Milele yakabidhi vifaa kwa Hospitali ya Chake Chake.

TAASISI ya Milele Zanzibar Foundation Pemba, imekabidhi mashine ya kuchemshia vifaa vya upasuwaji na nguo(auto clave), pamoja na mashine ya kufulia nguo vyote vikiwa na tahamani ya shilingi Milioni 14 kwa uongozi wa Hospitali ya Chake Chake. Vifaa hivyo vilivyokabidhiwa ni mashine ya auto clave yenye thamani ya shilingi Milioni 12 na mashine ya kufulia nguo yenye thamani Milioni mbili. Akuzungumza katika hafla ya kukabidhi mashine hizo, kwa uongozi wa hospitali ya Chake Chake, mratib wa Taasisi ya Milele Ofisi ya Pemba Abdalla Said Abdalla, alisema taasisi hiyo imo katika harakati za kusaidia jamii katika kuwakomboa na umasikini. Alisema Milele imekuwa imejikita katika kusaidia sehemu tafauti ikiwemo elimu, Afya, Uchumi, ili kuwahikisha wananchi wananufaika na uondokana na...
Video: RC Kusini Pemba “Acheni kujichukulia sheria mikononi”.
Kitaifa, Sheria

Video: RC Kusini Pemba “Acheni kujichukulia sheria mikononi”.

  Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba ambae pia ni Mwenyeiti wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoa Mh. HEMED SLEIMAN ABDALLA amewataka wananchi kuacha tabia ya kuchukuwa sheria  mikononi mwao kwani vitendo hivyo  vinaweza kuhatarisha uvunjifu wa amanii nchini. Mkuu wa Mkoa huyo ametowa wito huo huko ofisini kwake Chake Chake wakati akizungumza na ZBC   kufuatia tukio la kijana mmoja kuwapinga mapanga watu watatu huko katika kijiji cha Kangagani Wete. Amesema katika kipindi hichi cha kampeni kuelekea uchaguzi mkuu kumekuwa na mikusanyiko ya watu mbali mbali hivyo kwa wale ambao watahudhuria katika kampeni hizo hawana budi  kuhakikisha wanaendelea kudumisha amani  na utulivu kwa usalama wao na taifa kwa ujumla. Kwa upande wake kamanda wa polisi Mkoa wa Kusini Pemba Msaidizi kamis...