Friday, October 18

Kitaifa

Wagombea CCM Jimbo la Chonga wanadi sera zao.
Kitaifa, Siasa

Wagombea CCM Jimbo la Chonga wanadi sera zao.

WAGOMBEA Ubunge na Uwakilishi Jimbo la Chonga Wilaya ya Chake Chake, kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) wamesema iwapo wananchi watawapa ridhaa ya kuongoza jimbo hilo, watahakikisha wanashirikiana katika kupeleka maendeleo pamoja na kutatua kero zote zainazowakabili wananchi wa jimbo hilo. Wagombea hao wamesema kuwa kwa sasa wanasubiri ridhaa za wananchi tu, ili kuanza harakati zakulibadilisha jimbo hilo ambalo kwa miaka mingi lilisahauliwa na viongozi wa jimbo waliokuwepo. Wakizungumza katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni za jimbo hilo, huko katika uwanja wa Mpira wa Skuli ya Pujini Wilaya ya Chake Chake, zikiongozwa na meneja wa Kampeni za CCM Mkoa wa kusini Pemba Mohamed Aboud Mohamed. Mgombea Ubunge wa jimbo hilo Juma Mohamed Juma, alisema iwapo atapata ridhaa ya kuwa ...
VIDEO:Watu watatu wajeruhiwa kwa panga.
Kitaifa

VIDEO:Watu watatu wajeruhiwa kwa panga.

Watu watatu wakaazi wa Kangagani katika Wilaya ya Wete wamelazwa katika Hospitali ya Vitongoji Chake Chake baada ya kujeruhiwa kwa  panga wakati wakiwa msikitini katika ibada ya swala ya alfajiri ya leo. Akizungumzia kuhusu tukio hilo  Daktari dhamana Hospitali ya Vitongoji Dr. Sharif Khatib amesema amewapokea majeruhi hao majira ya saa kumi na mbili  asubuhi na kupatiwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Juma Sadi amesema Jeshi la polisi linaendelea na upelelezi wa tukio hilo . Nae Mkuu wa Wilaya ya Wete kamanda Mohammed Mussa Mkobani amewataka wananchi wa Wilaya hio kuwa na amani huku Serikali ikishirikiana na vyombo vya sheria ili kuhakikisha muhusika wa tukio hilo anachukuliwa hatua. Kwa...
Wapigwa mapanga msikitini.
Kitaifa, Sheria, Siasa

Wapigwa mapanga msikitini.

  NA MWANDISHI WETU.     WAZIRI wa nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Mohamed Aboud Mohamed, amesema katika kipindi hichi cha kuelekea uchaguzi mkuu sio vizuri mtu kuchukua sheria mikononi mwake jambo ambalo linaweza kupelekea uvunjivu wa amani ndani ya nchi. Aliyasema hayo katika Hospitali ya Vitongoji mara baada ya kuwatembelea na kuwafariji majeruhi ambao walipigwa mapanga alfajiri ya kuamkia jana huko Kangagani Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba. Alisema, mtu yoyote haruhusiwi kuchukua sheria mikononi mwake kwani Serikali na vyombo vya usalama vipo macho na vinaendelea kufanya ulinzi katika maeneo yote ya nchi. Alieleza, kwa sasa msako mkali utaendelea kufanyika na kwa yoyote ambae atashiriki kwa njia moja ama nyengine kuharibu ama...
VIDEO: Wagombea jimbo la Kiwani wanadi sera zao.
Kitaifa, Siasa

VIDEO: Wagombea jimbo la Kiwani wanadi sera zao.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kiwani  katika Wilaya ya Mkoani ndugu Rashid Abdalla Rashid  amewataka wananchi wa Jimbo hilo kumchagua na kuendelea kukipigia kura Chama cha Mapinduzi  ili kiweze kuwaletea maendeleo wazanzibar na Watanzania kwa ujumla. Ndugu Rashid ameyasema hayo huko Mwambe wakati wa uzinduzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi katika jimbo la Kiwani. Amesema katika uongozi wa awamu ya saba inayomalizia kuna miradi mingi ya maendeleo imeekezwa kwa ajili ya kuwaondoshea kero wananchi hivyo ni vyema kuendelea kukiweka madarakani chama cha mapinduzi ili wananchi wazidi kunufaika na maendeleo hayo. Naye mgombea  wa uwakilishi wa jimbo la Kiwani ndugu Mussa Foum Mussa amesema katika kipindi kilichopita wakati akiwa mwakilishi wa jimbo hilo alifanikiwa kusimamia upatiukan...