DK. Shein aweka jiwe la msingi Pemba.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, amesema kuwa sula la viwanda kwa Zanzibar ni suala la miaka mingi sana, kabla ya Mapinduzi matukufu ya mwaka 1964 na baada ya Mapinduzi, ikiwemo viwanda vidogo vidogo, vya kati na vikubwa.
Alisema viwanda hivyo vilikuwa vya sabuni, usumba, mafuta ya nazi, viwanda vya soda, maziwa, Mapinduzi ya mwaka 1964 ndio yaliobadili maendeleo hayo.
Dk.Shein aliyaeleza hayo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mikoa miwili ya Pemba, mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa kiwanda cha kusarifia Mwani uliokwenda sambamba na Uzinduzi wa eneo la Viwanda Chamanangwe II Mkoa wa Kaskazini Pemba.
“Zanzibar ilikuwa imenawiri kwa viwanda vidogo vidogo, ikiwemo viwanda vya maziwa, mterekta, soda, kiwanda c...