Friday, December 27

Kitaifa

DK. Shein : CCM haikukosea kumteua dk: Hussein Ali Mwinyi kugombea nafasi ya urais wa Zanzibar.
Kitaifa, Siasa

DK. Shein : CCM haikukosea kumteua dk: Hussein Ali Mwinyi kugombea nafasi ya urais wa Zanzibar.

NA HAJI NASSOR, PEMBA RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Mapinduzi Mhe: dk: Ali Mohamed Shein, amesema CCM haikukosea kumteua dk: Hussein Ali Mwinyi kugombea nafasi ya urais wa Zanzibar, kwani anasifa ya uchapakazi uliotukuka, ambao wagombea wa vyama vyengine hawana. Dk: Shein, ameeleza hayo uwanja wa Gombani kongwe wilaya ya Chake Chake Pemba, alipokuwa akizungumza na mamia ya wanaCCM na wananchi wengine, kwenye uzinduzi wa kampeni kwa chama hicho, na kumnadi mgombea huyo wa urais wa Zanzibar. Alisema, CCM daima imekuwa ikiteua wagombea wake wa nafasi mbali mbali wenye sifa bora za kufanya kazi kwa nidhamu, uhodari na usiopendelea mtu wala kundi lolote, na kuwaomba wananchi kumchagua kwa kishindo mgombea huyo. Alieleza kuwa, mgombea huyo wa urais wa Zanzibar kwa ...
Mgombea ubunge Ole kupitia cha UMMA kuving’arisha vikundi vya wanawake akishinda
Kitaifa, Siasa, Wanawake & Watoto

Mgombea ubunge Ole kupitia cha UMMA kuving’arisha vikundi vya wanawake akishinda

IMEANDIKWA NA HAJI NASSOR, PEMBA MGOMBEA Ubunge wa Jimbo wa Ole kwa tiketi ya chama cha Ukombozi wa UMMA, Maryam Saleh Juma, amesema iwapo atapewa ridhaa ya kuliongoza jimbo hilo, atahakikisha vikundi vya ushirika vya wanawake anavipatia mitaji, na kuwa kimbilio kwa wengine wanaobeza. Alisema, bado kundi kubwa la wanawake wanaonekana kutoviunga mkono vikundi vya ushirika, kwa kule kukosa mitaji na mikopo yenye masharti nafuu, ambapo kama akipata ridhaa hilo ndio kipaumbele chake. Mgombea huyo ubunge ameyaeleza hayo, alipokuwa akizungumza na pembatoday, juu malengo na azma yake ya kuomba nafasi hiyo Jimboni humo. Alisema, hamu na ari yake ya kuwawezesha wanawake ipo ndani ya moyo wake, na ndani ya mwaka mmoja baada ya kuingia bungeni, wanawake wa Jimbo hilo watakuwa na maish...
Mahakama yamrejesha uraiani aliyedaiwa kumuingilia mlemavu Pujini
Kitaifa, Sheria, Wanawake & Watoto

Mahakama yamrejesha uraiani aliyedaiwa kumuingilia mlemavu Pujini

IMEANDIKWA NA HAJI NASSOR, PEMBA MAHAKAMA ya mkoa Chake Chake, imemuachia huru, kijana Abdalla Khatib Abdalla miaka 25 wa Pujini, aliyekuwa akituhumiwa kumuingilia mwanamke mwenye ulemavu wa akili, baada ya mahakama hiyo kubaini utata juu ya eneo alililodaiwa kuingiliwa mwanamke huyo. Hakimu wa mahakama hiyo Luciano Makoye Nyengo, alisema kuwa, amelazimika kumuachia huru mtuhumiwa kwa vile, shahidi mmoja alidai mwanamke huyo aliingiliwa kichani tena chini ya Muwembe. Alisema, ilipofika wakati wa shahidi muathirika ambae ana ulemavu wa akili, aliimbia mahakama hiyo kuwa, aliingiliwa na mtuhumiwa ndani ya nyumba eneo la Pujini na sio kichakani. “Shahidi mmoja alidai kuwa, tukio la kuingiliwa kwa mwanamke huyo lilifanyika kichakani, ingawa alipokuja muathirika wa tukio, aliiel...