Tatizo la mgao wa maji Zanzibar linatarajiwa kuwa historia.
NA ABDI SULEIMAN.
MWENYEKITI wa Bodi ya wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Balozi Mstaafu na Meja jenerali Mstaafu Issa Suleiman Nassor, amesema baada kukamilika kwa miradi ya Maji Uviko 19 tatizo la mgao wa maji nchini linatarajiwa kuwa historia.
Alisema miradi hiyo uchimbaji wa Visima vipya 38 na ujenzi wa matangi ya maji 10, ambapo kukamilika kwake kutaweza kuliondosha kabisa tataizo la mgao wa maji nchini.
Mwenyekiti huyo aliyaeleza hayo mara baada ya kuamiza ziara ya kutembelea miradi hiyo ya maji ya Uviko 19 Kisiwani Pemba, ili kuona imefikiwa hatua gani.
Alisema kwa sasa wananchi wanapaswa kukaa katika hali nzuri na kusubiri mabadiliko makubwa katika sekta ya maji, hivyo aliwasihi wananchi kuwa makini katika matumizi ya maji kwa kuacha upotevu wa maji...