Thursday, January 16

maji

TUNDAUWA wapatia vifaa vya maji
Kitaifa, maji

TUNDAUWA wapatia vifaa vya maji

NA HANIFA SALIM. ZAIDI ya shilingi Milioni 45,000,000/= zimetolewa na taasisi ya Ifraji Zanzibar Foundation, kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kusambazia huduma ya maji safi na salama kwa kijiji cha Tundauwa Wilaya ya Chake chake Pemba. Akizungumza katika makabiziano ya vifaa hivyo, Meneja wa Taasisi ya Ifraji Zanzibar Foundation Pemba Abdalla Said Abdalla, alisema vifaa hivyo ni pamoja na mipira yenye urefu wa kilomita tatu, paipu za nchi mbili na tatu na viungo vyake vya kufungia. Alisema Ifraji ni taasisi yao ndogo imedhamiria kusaidia jamii kwa kiasi kikubwa, ambao lengo lake ni kuhakikisha wananchi wote hasa maeneo ya vijijini wanapata huduma ya maji safi na salama. Alieleza, maji ni kitu muhimu kwa binaadamu hata miti, ambapo Ifraji imekipa kipaumbele chake kimoja, ik...