Monday, January 27

Makala

MCHANGO WA WAANDISHI NA  VYOMBO VYA HABARI  KWA VIONGOZI  WANAWAKE.
Kitaifa, Makala

MCHANGO WA WAANDISHI NA VYOMBO VYA HABARI KWA VIONGOZI WANAWAKE.

FATMA Juma  Khamis  Diwani  wa  Tibirinzi  Chake chake   yenye jumla ya wakazi 11,089 wanawake ) 5,785  (wanaume)  5,304  ambaye  anawachukulia waandishi wa habari  na vyombo vya habari kwake kama ndugu zake wa damu  . Hii ni kutokana na yeye kufanya kazi  kwa ukaribu zaidi na wanahabari kabla ya kuzianza harakati hizi za siasa na uongozi mnamo mwaka  2000. Fatma Juma Khamis mwenye umri wa maiaka 42 Mzaliwa na mkaazi wa  Msingini Chake  Chake  Mkoa wa Kusini Pemba mtaa wenye  idadi ya wakazi 2,748 (wanaume ) 1,286 (wanawake) 1,462  na kaya 517 ,Mke na mama wa watoto 4, mwenye elimu ya kidato cha 4 ambae licha ya nafasi hiyo ni mtaalamu katika masuala ya utoaji wa huduma za kijamii ikiwemo ushauri masuala ya afya  na mazinagira.   (more…)
PPC kuvitangaza vivutio vya Utalii kISIWANI Pemba , Kuunga mkono kauli ya Rais wakiwa kama waandishi   ni wajibu wao.
Makala

PPC kuvitangaza vivutio vya Utalii kISIWANI Pemba , Kuunga mkono kauli ya Rais wakiwa kama waandishi   ni wajibu wao.

Na Maryam Talib – Pemba. HAKIKA kuweza nikujiwezesha hakuna kitu kinachokuja bila ya kujishuhulisha hayo ni maneno ya bwana  Hamad Salim mwenye umri wa miaka (65) alipoamua kuanzisha shamba lake la viungo lililopo sehemu moja inayopatikana Gando katika shehia ya Gando mkoa wa  kaskazini Pemba. Kilimo cha viungo ni fursa adhimu iliyopuuzwa na kufichika katika  Kisiwa cha Pemba ambayo kama ingetumiwa vyema na wakaazi wa kisiwa hichi ingekuwa na manufaa makubwa hasa hasa kwa  utalii wa ndani  na kwa wananchi wa kawaida . Hata hivyo kuna fursa moja muhimu iliyofichika kwa wakaazi wa kisiwa cha Pemba ambayo takribani miaka saba sasa anaitumia Bwana Hamad Salim wa Gando nayo ni ya kilimo cha viungo ikiwamo kilimo cha vanilla, hiliki, midalasini, tangawizi, majano, pilipili manga na ...
ZAINA FOUNDATION MKOMBOZI WA WANAWAKE KATIKA KUTUMIA DIGITALI TANZANIA.
Makala

ZAINA FOUNDATION MKOMBOZI WA WANAWAKE KATIKA KUTUMIA DIGITALI TANZANIA.

  NA, AMINA AHMED MOH’D-PEMBA.  ZAITUNI Abdulkarim Njovu ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Zaina Foundation inayotetea haki  ya kutumia mitandao ya kijamii kwa wanawake Tanzania.  Taasisi hiyo ambayo makao makuu yake makuu yake ni Dar es Salam  ilianza harakati hizo  mwaka 2017  na kufika Zanzibar  mwaka 2022. Zaituni alisema walifikia uamzi wa kuwa na hio taasisi baada ya kugundua kuwepo changamoto nyingi, ikiwemo ya ukatili wa kijinsia mtandaoni. Vile vile zipo changamoto za kiuchumi, kiwango cha chini cha elimu ya matumizi sahihi ya mtandao na wanawake kidogo kutumia haki hiyo . Vile vile sheria sio rafiki kwa mwanamke kukingwa anapofanyiwa udhalilishaji mtadaoni. Kwa mujibu wa takwimu  za sensa ya watu na makazi za  mwaka 2022 Tanzan...
Zawadi: Mwakilishi wa Konde anaepambania kuzitatua changamoto za wananchi.
Makala

Zawadi: Mwakilishi wa Konde anaepambania kuzitatua changamoto za wananchi.

‘Asema, watu wayasemee mazuri anayoyatekeleza sio kumbeza’ NA ZUHURA JUMA, PEMBA "NIMECHIMBA visima nane katika Jimbo langu, visima sita ni vipya na viwili vilikuwepo zamani lakini vilikuwa havitumiki tena kutokana na uchakavu," si maneno ya mtu mwengine bali ni ya mwakilishi wa Jimbo la Konde Zawadi Amour Nassor. Zawadi ni mwanamke anaepambania kuzimaliza changamoto ndani ya jimbo lake ambazo zilikuwa zikimkosesha usingizi kabla ya kuwa kiongozi. Mama huo wa makamo anaendelea kutimiza malengo yake aliyojiwekea baada ya kuingia kwenye chombo cha kutoa maamuzi, ambayo ni ndoto yake ya muda mrefu. Katika kipindi hiki cha muda mfupi cha uongozi wake, amefanya mambo mengi ikiwa ni pamoja na uchimbaji wa visima, hali ambayo imewapunguzia usumbufu wananchi hasa wanawake na wa...