MAKALA VIDEO: SAUTI YAO, jee! unataka kujua leo itasikika sauti ya nani katika makala haya?
NA KHADIJA KOMBO-PEMBA.
Kukomesha umaskini wa mtoto ni muhimu sana kwa ajili ya kutoa haki kwa kila mtoto na kwa ajili ya mustakabali wa jamii na Taifa kwa ujumla.
Ikiwa hautashughulikiwa kwa ukamilifu, umaskini utawazuia watoto kufikia ukuaji wao kamili na kudumaza ustawi wa taifa, ikiwa ni pamoja na maendeleo ya ‘Dira ya Tanzania ya mwaka 2025'.
Ili kupima umaskini wa mtoto kwa ufanisi, mahitaji mengine muhimu kwa ajili ya ustawi wa mtoto, mbali na kipato cha kaya, yanatakiwa kujumuishwa.
Hivyo,Tanzania imeandaa njia ya kupima umaskini wa mtoto kwa ukamilifu ambayo ni mahsusi kwa nchi.
Kipimo hicho kinazingatia uwezekano wa mtoto kupatalishe, huduma za afya, ulinzi na usalama, elimu, habari, usafi wa mazingira, maji na makaazi.
Upimaji sahihi wa umaskini w...