NA ABDI SULEIMAN.
AMANI, Umoja, Upendo na Mshikamano haya ndio maneno mbayo, siku hizi yamekuwa yakizungumzwa kwa sana, katika maeneo mbali mbali hata nyumba za ibada.
Hata Waasisi wa taifa hili walikuwa wakipinga suala zima la ubaguzi na kuhimiza umoja, mshikamano na upendo kwa wananchi, kitu ambacho kinapaswa kuendelezwa.
Historia inaonyesha Zanzibar mfumo wa vyama vingi Zanzibar ulianza mwaka 1992, mwaka 2005 baada ya sitofahamu za uchaguzi Rais Dk.Amani Abeid Karume alianzisha mazungumzo ya kuwepo kwa maridhiano ya serikali ya Umoja wa Kitaifa na Maalim Seif Sharif Hamad 2009, ili kuondosha uhasama wa kisiasa uliokuwepo.
Marehemu Abubakar Khamis Bakar aliyekuwa mwakilishi wa jimbo la Mgogoni, aliwasilisha hoja binafsi katika baraza la wawakilishi kulitaka baraza hilo ku...